Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Mkuu wa shule Jamia Urwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa katika msikiti wa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Januari 27, 2023
Mahubiri ya 1: Misikiti ni sehemu ya mahusiano ya kijamii na Sehemu Muwafaka kwa ajili ya kuufikia utukufu wa kiroho
Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika misingi ya Uchaji Mungu.
Tambueni kuwa ucha Mungu ni mjumuiko wa mipango na mikakati kutoka kwa Mwenyezi Mungu yenye kumlinda mwanadamu.
Sehemu muhimu zaidi ya maisha ya mwanadamu ni maisha yake ya kijamii, na Sehemu zingine zote hulelewa chini ya maisha haya ya kijamii.
Ikiwa maisha ya kijamii hayatahifadhiwa, basi maisha ya mtu binafsi na nyanja zingine za maisha hazitakuwa na usalama. Kuna Taqwa iliyoanzishwa kwa ajili ya maisha binafsi na yale ya kijamii ya mwanadamu.
Katika aya ya 200 ya Suratu al-Imran.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa.
Kundi linalohutubiwa ni jamii ya waumini ili waweze kupata subira, na kuwasaidia wengine, kufanya Murabeta na Taqwa ili wapate mafanikio. Taqwa katika nyanja ya kijamii ni sawa na ulinzi katika sehemu hiyo. Sehemu kubwa ya maisha yetu inatumika katika nyanja ya kijamii kwa hivyo hatari zaidi iko hapa.
Taqwa ni kinga dhidi ya vitisho kama hivi ambavyo ni vya namna ambayo hukatisha uhai wa mwanadamu. Wakati mwanadamu ameagizwa kwa ajili ya Murabeta na vilevile ramani ya vitendo imewasilishwa kwa ajili ya jambo hili. Kuna Murabeta unahitajika katika jamii, miongoni mwao waumini, pamoja na viongozi wenye kuongoza vituo vyenye kuwapa watu mwongozo.
Sehemu yoyote inayokuja na uhusiano, hukumbwa na hatari . Mahusiano ya kijamii ni muhimu sana kama vile mahusiano ya kifamilia, kati ya matabaka, uhusiano wa kisiasa, masuala ya ulinzi yote haya ni sehemu ya Murabeta.
Miongoni mwa mambo haya Murabeta muhimu kwa mwanadamu ni kama vile kituo chake cha kidini. Sio vile vituo ambavyo tumevitengeza sisi wenyewe, bali ni vile ambavyo Mwenyezi Mungu ametuelekeza kwavyo.
Kama ambavyo Kaaba ni kituo cha kimataifa cha maendeleo ya Ummah.
Ndivyo misikiti inakua ni vituo ambavyo vimeundwa kwa ajili ya mahusiano ya kijamii. Tunaichukulia misikiti kua ni kwa ajili ya mambo ya ibada na kiroho tu kama vile Sala. Tunaichukulia Sala kuwa ni ya kiroho ambayo tusipoweza kuitekeleza tunaiona kuwa haina maana yeyote.
Kipengele kimoja cha msikiti ni kubwa na uhusiano na Mwenyezi Mungu kupitia njia ya ibada, lakini haya sio matumizi ya pekee ya msikiti. Ni moja kati ya faida za msikiti, lakini uhusiano na Mwenyezi Mungu unaweza kuanzishwa hata majumbani pia, na ni bora ikawa matendo ya ibada yatafanywa katika faragha.
Kwa haraka haraka ni vigumu kuanzisha uhusiano na Mwenyezi Mungu kwakua mwanadamu anaweza kupoteza umakini katika jambo lile.
Tunaweza kuona kwamba tumekusanyika kwa ajili ya sala ya Ijumaa na kwamba kuna mambo ambayo yameondoa mawazo yetu. Kitu pekee ambacho hatuzingatii ni Mahubiri. Watu waliokaa kwa karibu, kuwavutia wale wote wanaokuja baadae.
Tunaweza kusema basi ni bora mwanadamu akae peke yake ambapo ni yeye na Mwenyezi Mungu tu pasi na kuwepo kitu chengine. Anaweza fikia daraja za juu za Kiroho, lakini tunaona kwamba mwanadamu anazuiwa kufanya hivi mapangoni. Uhusiano na Mwenyezi Mungu huimarika unapokaa baina ya watu.
Sharti la uhusiano na Mwenyezi Mungu ni kuanzisha uhusiano baina yenu nyinyi kwanza.
Unapoanzisha uhusiano baina yako na watu basi unapata mafungamano na Mwenyezi Mungu. Mitume wamekuja wakiwa miongoni mwa watu.
Watu hawakuwa na maelewano mazuri baina yao na Mwenyezi Mungu hakua nao karibu nao. Mitume wakaja kuwaunganisha na kisha wakawaunganisha na Mwenyezi Mungu.
Huu ndio utaratibu wa dini. Ambayo ndio mojawapo ya kazi muhimu ya msikiti, vituo ni sawa na Sehemu ya kuanzisha uhusiano kati yao.
Msikiti ni sehemu ya kijamii ambapo unapaswa kuanzisha mkusanyiko katika Swala. Jamaat (swala ya jamaa) maana yake ni kukusanyika pamoja.
Ijumaa ni siku ya mkusanyiko na msikitini ndio sehemu yake.
Siku yenyewe na msikiti vyote vinahesabika kua ni Jumah, kwa sababu maana yake ni siku na mahali pa mkusanyiko. Kwa hivyo Kwanza anzisheni uhusiano kati yenu.
Na Madhumuni ya mahusiano haya ni kupata uhusiano na Mwenyezi Mungu. Siku ya Ijumaa tunaamriwa kukusanyika pamoja na hata ikibidi kusafiri masafa basi iwe ni baada ya Swalah ya Ijumaa. Kisha baada ya kukusanyika na kuswali Quran inasema mnaweza kutawanyika katika ardhi.
Siku ya Ijumaa ni siku ya mkusanyiko unaopaswa kufanywa katika sehemu iliyofaradhishwa ambayo ni msikiti. Swala za kila siku mara tano ni za maeneo mengine ila katika Ijumaa hua kunakuwepo na mkusanyiko mkubwa ambapo watu wanapaswa kukusanyika katika msikiti wa Kati.
Mkusanyiko huu ndilo kusudiovna kupitia hili unaweza kufanya safari yako kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Mkusanyiko huu unabaraka ndani yake na katika mkusanyiko huu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko pamoja nao kama jamii na si kwa mtu binafsi.
Katika mkusanyiko huu tumepewa baraka mbili, mojawapo ni Swala na ya pili ni msikiti. Kuna nukta ya kiroho katika haya, lakini tunazingatia hii tu kimakusudi.
Tumeambiwa tuwe makini sana katika Swala na tusigeuze mazingatio yetu hata kwa muda mfupi. Nani anaweza kulifikia hili? Huenda ukaweza kulifanya kutokana na upendeleo maalum kutoka kwa Mwenyezi Mungu lakini unaweza kufikia kusudio hilo kwa kukusanyika.
Katika mkusanyiko huu mjadala ufanyike kwa mujibu wa jambo hili. Mkutano wa Ijumaa kila wakati unapaswa kutoa matokeo mapya na sio kwamba jambo lile lile hurudiwa kila Ijumaa.
Je, umechukua hatua mpya kila Ijumaa katika uhusiano wako na jamii? Ikiwa umebaki pale ulipokuwa, licha ya kuhudhuria Swalah ya Ijumaa katika maisha yote, basi hujapata faida yoyote kutokana na Swalah ya Ijumaa.
Vile vile katika Swala, kama Ali (a) anavyosema kwamba mtu ambaye siku zake mbili zinapita akiwa yuko hali ileile (hajaongeza chochote) basi anahesabika kua yuko katika hasara na udanganyifu. Kwa hivyo vipi ikiwa wiki mbili, miezi, miaka na maisha yote yanapita ukiwa katika hali ile ile, ni sawa na kua umelaaniwa.
Ukizingatia wanabiashara ulimwenguni , utagundua kua kila wakati wanataka kupiga hatua moja mbele. Unapompata mfanyabiashara hajapiga hatua yeyote katika biashara yake basi utapata ya kwamba si mwenye furaha.
Mwenyezi Mungu ametoa ramani ya Murabeta ( muungano) kama vile Msikiti, Sala, Hija na sala ya Ijumaa. Kisha kuna uhusiano pamoja na kiongozi. Tunapaswa kulifahamu lengo hilo la mkusanyiko huu.
Isiwe kwamba tunahudhuria tu na kupitisha wakati. Mwanadamu anaalikwa pamoja na kila mtu kufanya jambo fulani. Riwaya tuliyoitaja hapo kabla kwamba watu wanapohudhuria swala ya Ijumaa huandikiwa alama za kuhudhuria . Wale wanaokuja wa kwanza hupata daraja za juu.
Baadhi ya waumini wetu huzingatia sana kwamba watakapohudhuria basi sala iwe imeanza; kwa maana kwamba hatofika kwa wakati. Vilevile Malaika pia nao watakufanya usubiri katika malipo yako.
Riwaya inaeleza kua pepo yako inaandaliwa kwa mujibu wa maandalizi unayoyafanya kwa ajili ya sala ya Ijumaa. Ukweli huu nimeuelezea kwamba pepo na kuzimu sio miji tofauti ambayo tutahamishiwa huko kama makazi ya kuhama.
Mambo Tunayatengeneza hapa na pazia tu ndio zitainuliwa ili kuona kile tulichojitengenezea. Katika mila wakati mwamini mwadilifu anaingia kwenye ulimwengu wa kaburi, ambapo roho huenda nyuso fulani nzuri zimemzunguka.
Uso wa kwanza mzuri zaidi huja karibu na kuuliza muumini amtambue. Muumini anasema sijawahi kusikia au kuona wala kuufikiria uzuri kama huo.
Hiyo picha inasema mimi ni sala yako, yaani ni kitendo chako tu. Kisha utambulisho wa nyuso zote ni Saumu, Hajj, mambo fulani ya haki. Haya yote ni matendo ya muumini.
Uso wa matendo katika Barzakh ni tofauti na ulimwengu huu. Ulimwengu huo ni tofauti. Chochote tunachochukua kutoka hapa ni paradiso yetu au kuzimu.
Mwenyezi Mungu ametupa ramani kamili ya maisha ambayo Quran imekuja nayo. Muundo wa Ummah unapaswa kuwa na umbo jipya kila siku na kila wiki. Kwa ajili ya Swalah hii ya Ijumaa na vilevile ibada ya Hija.
Na katika mambo haya Kuna hatari kubwa kama ambavyo kila sehemu ya mwili wa mwanadamu zipo katika hatari. Mwenyezi Mungu ametupa Njia za kujikinga na hatari hizi na ametuamrisha tujilinde na tulinde miili yetu na mioyo yetu na vilevile jamii zetu na kisha katika Aya hii kama inavyotueleza kua tuzilinde subira zetu na mahusiano na hawa.
Mwenyezi Mungu anawataka waumini wailinde Sabr yao, Rabetu ( muungano) wao kwa Taqwa. Kwanza ni vyema tutathmini ni vitisho gani. Na Kwa vile tumezama katika vitisho hivi hatutambui.
Ni sheria ya kifalsafa kwamba mwanadamu anapozama kwenye kitu huwa hajitambui. Kwa mfano kuna binti mmoja ambaye babake alikua muuza manukato alikwenda kwa mtengenezaji wa ngozi. Msichana huyo alisumbuliwa na harufu ya ngozi iliyokua pale. Basi Alilazimika kupaka marashi kwenye baadhi ya vitu ili kumaliza harufu ya ngozi. Baada ya wiki moja alimwambia mama mkwe wake kuwa harufu imekwisha.
Yule mama mkwewe akaniambia kuwa haijaisha lakini wewe ndio umeizoea. Unaweza kuona watu wakifanya kazi kwenye mifereji ya maji chafu ukashindwa wanavumilia vipi kumbe ni kwa sababu harufu ile wameizoea na hisia zao zimeisha. Hatari ambayo jamii ya Wapakistani imegubikwa nayo ni ya wanasiasa wachafu, utamaduni mbovu ambao sote kwa sasa tunaufurahia.
Hisia zetu zimeshazoea kuhusu mchafuko huu wa kijamii tunayoishi ndani yake. Quran inasema kwamba ukame tulionao na ukosefu wa mvua ni kwa sababu ya matendo ya watu walioyafanya na ufisadi. Tukiichambua jamii yetu basi unaweza kuona na kuhisi vitisho hivyo.
Mtu mgonjwa hatambui kwamba ugonjwa umeingia ndani yake lakini wengine wanaweza kutambua kwa kumtazama. Ikiwa tutachukua uchambuzi wa nje basi tunaweza kuona hali ya ndani ilivyo.
Kama kusimama nje ya mlango tazama chumba chako tunapoishi utaona hali ya ndani ya chumba ilivyo. Ili kuboresha jamii hii tunahitaji juwa na Taqwa.
Mwenyezi Mungu ameiweka Taqwa katika mfumo lakini Wapakistani hawakuona hilo kuwa muhimu. Walifikiri vyama vya kisiasa na mitaji mingine kuwa muhimu na kwamba tumefanikiwa.
Mwenyezi Mungu ameiweka Taqwa katika malezi ya jamii. Inabidi tuweke misikiti na kuasisi jamii kwa misingi ya Taqwa. Inamlinda mwanadamu na pia jamii kutokana na hatari.
Tunaweza kuona jamii za kila siku; makoloni yanafanywa kwa ulinzi. Vikosi vinatengenezwa kwa mipaka. Kila mwamini anawajibika kwa ulinzi wa nafsi yake na jamii. Aina hii ya Taqwa inafunzwa katika vitabu au katika masomo mengine.
Katika Fiqh hakuna somo la Taqwa kwa sababu Fiqh inazingatia amri ya Ittaqu pekee ni. Kutoka kwa ‘Akimus Salaat’, ndio kitabu cha swala kilianzishwa.
Kwenye aya ya Taharat, kitabu cha Taharat kilitengenezwa, kwa maana aya ya hajj kitabu cha ibada za hajj kilitoka. Lakini Ittaqu ilikuwepo mara nyingi sana lakini Fiqh haikuifanya kuwa somo. Wanachuoni wa maadili waliipeleka Taqwa mahali pengine, kwa sababu hiyo jamii haina Taqwa.
Hii ndio sababu hatari hizi zimekuja kwa jamii. Kama nilivyosema kabla ya Uimamu kuwekwa katika mpango wa mwongozo, tuliutoa Uimamu kutoka kwenye mpango huo na tukapanda kwenye mimbari kwa ajili ya mihadhara. Hivyo Imamu wetu si kiongozi, mtawala hachukuliwi bali ni Tawassul.
Mwenyezi Mungu amemfanya Imamu kwa ajili ya utawala na tumemtumia kwa ajili ya Tawassul, tunahitaji viongozi wachafu wa kisiasa kwa ajili ya utawala na kufikiri kua tunaweza kuendesha serikali bila Imamu, tunaweza kumfanya Saddam, bin Salman kama Hakim.
Mwenyezi Mungu amemuweka Imam ili msiwafanye mafaasid (waovu) kuwa Maimamu. Mamlaka ya maisha yako yako kwa Maimam na sio njia ya kutafuta. Umechukua haki za Uimamu na kuwapa majambazi wachafu wa kisiasa. Na kisha kukaa kila Jumanne kusoma dua ya tawassul.
Tunasema katika tawassul kwamba tunakuleteeni mbele yenu haja zetu. Hii ina maana lengo la msingi ni matamanio yetu na ili kupata yale yatakayokubaliwa tunakuweka mbele ya Mwenyezi Mungu ili kuyatimiza hayo. Sisi wenyewe tunasema kuwa tunakuwasilisha kwa Mwenyezi Mungu kwa matamanio yetu.
Mwenyezi Mungu ameviwasilisha kwa ajili ya mwongozo wetu, wokovu. Mwenyezi Mungu aliwatuma kama walinzi wa maisha yetu na akhera.
Wao ni nguzo za ubwana wa Mwenyezi Mungu. Tumemuweka Shahbaz Sharif mahali pa Uimamu. Inabidi tujenge umakini kuhusu dini na hasa kwakua tumeielewa Taqwa katika nyanja za kijamii na kisha baada ya hapo kuifanyia kazi.
Mahubiri ya 2: Kujipenda na Kujitenga
Katika msemo nambari 113, Imam Ali (a.s) anawasilisha mfumo mzuri kwa waumini.
وَقَالَ (عليه السلام):لاَ مَالَ أَعْوَدُ مِنَ الْعَقْلِ، وَلاَ وَحْدَةَ أَوْحَشُ مِنَ الْعُجْب، وَلاَ عَقْلَ كَالتَّدْبِيرِ، وَلاَ كَرَمَ كَالتَّقْوَى، وَلاَ قَرين كَحُسنِ الخُلْقِ، وَلاَ مِيرَاثَ كَالاْدَبِ، وَلاَ قَائِدَ كَالتَّوْفِيقِ، وَلاَ تِجَارَةَ كَالْعَمَلِ الصَّالِحِ، وَلاَ رِبْحَ كَالثَّوَابِ، وَلاَ وَرَعَ كالْوُقُوفِ عِنْدَ الشُّبْهَةِ، وَلاَ زُهْدَ كَالزُّهْدِ فِي الْحَرَامِ،ولاَ عِلْمَ كَالتَّفَكُّرِ، وَلاَ عِبَادَةَ كَأَدَاءِ الْفَرائِضِ، وَلاَ إِيمَانَ كَالْحَيَاءِ وَالصَّبْرِ، وَلاَ حَسَبَ كَالتَّوَاضُعِ، وَلاَ شَرَفَ كَالْعِلْمِ، وَلاَ عِزَّ كَالْحِلْمِوَلاَ مُظَاهَرَةَ أَوْثَقُ مِن مُشَاوَرَةٍ.
113. Amirul-Muuminin, amani iwe juu yake, amesema:
Hakuna mali yenye faida zaidi kuliko hekima, hakuna upweke ni mgeni kuliko ubatili, hakuna hekima ni nzuri kama busara, hakuna heshima kama hofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hakuna mshirika kama wema wa tabia, hakuna urithi kama ustaarabu, hakuna mwongozo. ni kama haraka, hakuna biashara ni kama matendo mema, hakuna faida ni kama malipo ya Mwenyezi Mungu, hakuna kujizuia ni kama kutotenda wakati wa shaka, hakuna kujiepusha na kukatazwa, hakuna elimu kama kufikiri, hakuna ibada. ni kama kutekeleza wajibu, hakuna imani ni kama staha na subira, hakuna kupata ni kama unyenyekevu, hakuna heshima ni kama elimu, hakuna nguvu ni kama subira, na hakuna msaada ni ya kuaminika zaidi kuliko kushauriana.
Majadiliano kuhusu Aql ni makubwa sana katika Quran na mafundisho ya ‘ujb’. Sentensi ya pili ni
وَلاَ وَحْدَةَ أَوْحَشُ مِنَ الْعُجْب
hakuna upweke ni mgeni kuliko ‘ujb’ ubatili
Mwanadamu ni wa kijamii na ni kiumbe ambacho hakiwezi kuishi bila uhusiano na wengine. Lakini wakati fulani mwanadamu anakuwa mwathirika wa upweke na kutengwa. Hii inaweza kutokana na kizuizi, nguvu, matatizo na wakati fulani gerezani ambapo mwanadamu ametengwa.
Hata gerezani ikiwa kuna wafungwa wengine sio adhabu kali hiyo. Lakini ikiwa mwanadamu amewekwa mahali ambapo hakuna mwanadamu mwingine ni ngumu sana.
Mfia-imani mmoja anasema kwamba nilipokamatwa mara ya kwanza, walimpa mateso makali zaidi kunifanya niungame chochote walichotaka.
Ningetamani kifo wakati huo ili nipate uhuru. Kisha anasema nilipata kimbilio ambapo niliwekwa gerezani peke yangu.
Aliwekwa kwenye chumba kidogo ambacho hakuweza kutoka. Kulikuwa hakuna mwanga, mlango wa chuma usio na kioo. Miale midogo ya mwanga ingeingia ndani ambayo ingemuonyesha kua ni mchana. Walimwekea chakula ndani na kupumzika ila yote yalifanyika ndani.
Baada ya siku kadhaa kupita akiwa katika upweke huo wa kutisha anasema nilichanganyikiwa. Niligonga mlango walinzi wakaja, nikawaambia wanitoe kwenye upweke huu na wanipeleke mahali pa mateso. Angalau naweza kuona au kukutana na binadamu mwengine, siwezi kuvumilia hili.
Kuna baadhi ya watu hutengwa katika jamii fulani au nyumbani kwa sababu mbalimbali. Wakati fulani kwa sababu ya kuchagua au wakati fulani kwa kushawishiwa.
Kutengwa kwa mwanadamu ni kugumu sana kwani yeye ni mwanadamu ambaye ni kiumbe wa kijamii. Ikiwa mtu atakua na uhusiano na Watu au jamii basi anaweza akaishia muda mrefu. Lakini Akiendelea kujitenga au kuishi pekeake basi atakufa.
Kwa kujitenga Imam Ali ( a.s) anasema kutengwa kwa kutisha zaidi ni UJB (kuona ya kwamba umejitosheleza) ambayo ina maana ya kujiona, au kujipenda. Anapenda nyumba yake, ubinafsi, na mzunguko wa maisha yake mwenyewe.
Mwanadamu anapenda vitu vya wanadamu kama vile kula na kuona matukio mengine tofauti. Kuna mengi anayapenda na asiyoyapenda ndani yake.
Mtu ambaye ni mgonjwa hujipenda na huwa katika hali ya kujisifu. Ukizungumzia Kaaba, msikiti, elimu, kitabu, Maimamu yeye hapendi chochote katika hivi. Anajipenda mwenyewe tu. Lakini muumini ni kinyume chake naye hupenda kitu sio kwa ajili ya nafsi yake tu lakini anapenda kila kitu kwa ajili ya wengine.
Kimaumbile mwanadamu anajipenda mwenyewe. Gnostiki anasema kwamba Mwenyezi Mungu ameuumba ulimwengu huu kutokana na upendo wake na kwa dhati yake mwenyewe.
Hakuna kitu kingine isipokuwa dhati ya Mwenyezi Mungu inayoweza kusimamisha mapenzi. Katika Hadith ya Qudsi Allah anasema, kwamba nilipewa hazina na nikakuza upendo wa kujieleza. Katika Hadithi hizi ya Qudsi mwalimu wetu angesema kuwa ni dhaifu katika usahihi lakini maudhui ni yake ni ya juu sana.
Dini nzima haiko hivi, kwa sababu Quran, mafundisho ya Ahlulbayt (a) yote yametoka kwa Mwenyezi Mungu pekee. Hatuwezi kupata dini nzima kutoka kwa Hadithi moja. Mwimbaji wa Qawwali anachukua neno moja kutoka kwa nathari na kisha anaendele
a kulirudia na kila mtu anakuwa na shauku. Wazungumzaji pia huchagua hadith moja na kuieleza dini nzima katika sentensi hiyo moja.
Qurani yote ni dini, vilevile maneno yote ya Mtume na Ahlulbayt (a) ni dini. Kujipenda ni katika sifa ya Mwenyezi Mungu na pia ni kuvipenda viumbe vyake, na ni kwa sababu vyote vinatoka kwa Mwenyezi Mungu.
Mwanadamu pia ana asilimia ya kujipenda lakini sio kwa kiwango kikubwa. Kwa sababu kujipenda huko kunasababisha harakati. Usemi mbaya wa kujipenda ni tofauti.
Ikiwa hutojipenda basi huwezi kujitunza mwenyewe, huwezi kuendeleza ukamilifu wowote ndani yako. Una upendo wa kibinafsi ambao hukupa rangi ambayo mimi sijakamilika na ninataka kuikamilisha. Kwa hivyo mwanadamu huchukua elimu.
Kujipenda huku ni katika Fitra ya mwanadamu, na dini haipingani na Fitra bali inaikuza. Katika Tarbiyat tunaanzisha vita dhidi ya Fitra. Mwanaume anapokuwa kijana, anahitaji ndoa na anaambiwa awe na Taqwa. Kwa nini unamfanya aende kinyume na Fitra.
Akiwa na njaa unamlisha. Kwa kulea, kuikamilisha Fitra ya mwanadamu. Kuna mambo ndani ya mwanadamu ambayo mwanadamu anapaswa kupigana nayo. Mahitaji ya Fitra ya mwanadamu yasipigwe vita. Na wengine wanaitimiza kwa kufanya Haramu.
Ikiwa mwanadamu haipendi nafsi yake, basi je, aichukie? Hili ni kinyume na Aql na dini na halipo. Upendo huu ni mali ya maisha ya mwanadamu. Lakini kwa ajili ya mapenzi Mwenyezi Mungu ameweka mfumo wa udhibiti wa uongofu. Kujisifu sio kujipenda.
Kujipenda kunampeleka mwanadamu kwenye ukamilifu na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Wakati fulani kujipenda kunakuwa tamaa. Quran inasema kwamba Mwanadamu anakuwa na tamaa ya mali, nafsi, wanawake, madaraka.
Hizi ni zile usahihi katika dini ambazo tunaziwasilisha kwa namna ya kutia shaka. Katika kujionyesha, tunasema kwamba nikipenda kitendo changu kitakuwa cha kujionyesha.
Hii si kweli. Maulana mmoja asingeongoza sala. Angeweza kusema kwamba itakuwa kujionyesha kama mimi kusimama mbele.
Ikiwa mwanadamu anaelewa dini iliyopotoka basi hii inakuwa ni fikra ya kishetani. Kama vile ulimwengu unavyopaswa kuishi na kuhukumiwa vile vile, kwa hivyo yanapaswa kufafanuliwa.
Kujipenda sio kujipenda kwa maana hasi, lakini kuna vitendo fulani vinavyoifanya kuwa hasi, Ambayo Tutajadili baadaye.