“Zuliville Mandela”, mjukuu wa “Nelson Mandela” na mjumbe wa Bunge la Afrika Kusini alisema: “Nia thabiti ya Wapalestina kupata uhuru wa nchi yao imekuwa msukumo katika kuibua suala la Palestina katika duru za kimataifa.”
Zuliville Mandela ambaye alikwenda Istanbul kwa ajili ya kujadili na kuchunguza kadhia ya Palestina na uchokozi wa utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina amesema: Suala la Palestina daima limekuwa katika nyoyo za raia wa Afrika Kusini na halitasahaulika kamwe.
Aliongeza: Nelson Mandela, muasisi wa demokrasia ya nchi yetu, alitembelea Gaza kati ya 1995-1997 na akatangaza kwamba uhuru wetu hautakamilika bila uhuru wa watu wa Palestina.
Mjukuu wa Mandela alisema: Nelson Mandela alifanya makubaliano na Wapalestina katika suala hili, na kwa sababu hiyo, Afrika Kusini inaendelea kutetea suala la Palestina, na hata Mandela aliona mapambano ya Wapalestina kuwa suala muhimu zaidi la maadili katika zama hizi.