Mkoloni kizee Mfaransa atimuliwa rasmi nchini Burkina Faso

Serikali ya Burkina Faso imeamua kusitisha mkataba wa kijeshi ulioruhusu wanajeshi wa Ufaransa wafanye wanalotaka nchini humo. Mkataba huo wa kijeshi ulikuwa umeipa nchi ya Ulaya ya Ufaransa haki kubwa kuliko hata raia wenyewe wa Burkina Faso.

Ufaransa hivi sasa ina wanajeshi wake maalumu 400 katika nchi ya Afrika Magharibi.  Serikali mpya ya Burkina Faso imesema, imeamua kumtimua mkoloni huyo kizee wa Ulaya ili kulinda heshima na hadhi ya Burkina Faso na wananchi wake.

Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa serikali, Jean-Emmanuel Ouedraogo ambaye ameongeza kuwa, wananchi wenyewe wa Burkina Faso ndio wenye haki ya kujiamulia masuala yao, si mkoloni Ufaransa.

Mwaka 2018, Burkina Faso ilifikia makubaliano ya kijeshi na Ufaransa ambayo yaliruhusu wanajeshi wa nchi hiyo ya Ulaya kupelekwa nchini humo kwa kile kkilichodaiwa ni kupambana na waasi.

Lakini Jumamosi, ripoti za vyombo vya habari zilisema kuwa, serikali Ouagadougou imesitisha mkataba huo wa kijeshi na kuitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake nchini Burkina Faso katika kipindi cha mwezi mmoja.

Serikali ya Burkina Faso imetoa tangazo hilo siku moja baada ya Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa kuitaka serikali ya Ouagadougou kutoa maelezo kwa nini inataka wanajeshi wa Ufaransa waondoke huko Burkina Faso.

Ouedraogo amesema: “Tunacholalamikia leo ni makubaliano yanayoruhusu vikosi vya Ufaransa kuweko nchini Burkina Faso. Hii haina maana ya kumalizika uhusiano wa kidiplomasia kati ya Burkina Faso na Ufaransa. Katika hatua ya sasa, hatuoni jinsi ya kuwa wazi zaidi kuliko hivi.”

Uhusiano kati ya Ufaransa na Burkina Faso umeharibika sana tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Septemba 2022 katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *