Mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani CIA amsema Republicans ni chama hatari zaidi za siasa.
Gazeti la New York Post limechapisha makala ya uchambuzi iliyoandikwa na Callie Patterson ambaye amemnukuu mkuu wa zamani wa CIA Michael Hayden akisema, leo Warepublican wamekuwa hatari zaidi kuliko DAESH (ISIS), Al Qaeda na wengineo; wamekuwa watu hatari zaidi kuwahi kushuhudiwa mpaka sasa.
Jenerali huyo mstaafu wa jeshi la Marekani alichangia kuunga mkono ujumbe wa Twitter ulioandikwa Agosti 12 na mhariri mkuu wa gazeti la Financial Times Edward Luce ambaye alisema: “katika kipindi cha ufanyaji kazi wangu, nimeakisi na kuripoti idiolojia za vitendo vya ukatili na kufurutu mpaka, lakini sijawahi katu kukumbana na harakati ya kisiasa yenye mitazamo ya kipumbavu zaidi, hatari zaidi na duni zaidi kama ya Warepublican wa leo; hata wanaowakaribia wao.”
Hayden alikuwa mkuu za shirika la ujasusi la Marekani kuanzia Mei 2006 hadi Februari 2009.
Matamshi hayo ya mkuu huyo wa zamani wa CIA yamewashangaza na kuwashtua watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.
Wiki iliyopita, na kwa namna isiyo ya moja kwa moja, Hayden alisema, inapasa aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump anyongwe, kwa kuzihamishia nyaraka za siri za serikali kwenye makazi yake ya binafsi yaliyoko mjini Mar-a-Lago, Florida.
Mkuu huyo wa zamani wa CIA alitoa kauli hiyo ya kushtusha alipochangia maelezo ya mwanahistoria Michael Beschloss, aliyeonyesha picha za Julius na Ethel Rosenberg majasusi waliochukiza na kuandika, wawili hao walishtakiwa kwa kuzipeleka Moscow nyaraka za siri za nyuklia za Marekani na wakanyongwa Juni 1953. Hiden aliunga mkono andiko hilo kwa kusema: “inavyoonekana ni hatua sahihi.