Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada katika mkutano wa hadhara uliokua katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, huku wanamgambo wa al-Shabaab wakishambulia vituo vya polisi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waziri wa usalama wa mambo ya ndani wa Somalia alisema kuwa mnamo Jumatano asubuhi, wanamgambo wa al-Shabaab walishambulia vituo vya polisi na vituo vya ukaguzi vya usalama katika mji mkuu, Mogadishu.
Kundi la al-Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda, ambalo linalenga kupindua serikali kuu ya Somalia, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya serikali, ikiwa ni pamoja na shambulio la wiki iliyopita dhidi ya basi dogo lililokuwa limebeba wawakilishi wa uchaguzi.
Taarifa kuhusu waliojeruhiwa katika tukio hilo bado hazijatolewa. Abdullahi Noor alisema kuwa polisi watatoa taarifa zaidi kuhusu mashambulizi hayo.Al-Shabab hawajatoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.