Moncef Marzouki, rais wa zamani wa Tunisia amekosoa vikali hati ya makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baina ya Morocco na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kueleza kwamba, hilo lilikuwa ni kosa.
Faraan: Moncef Marzouki ameashiria mzozo na mvutano uliopo hivi sasa baina ya Algeria na Morocco na kuelezwa kwamba, kuingizwa utawala haramu wa Israel katika medani na uwanja wa hitilafu baina ya mataifa hayo mawili jirani ni mchezo mchafuu.
Kadhalika rais huyo wa zamani wa Tunisia ameeleza kwamba, kwa kuingizwa Israel katika uwanja huo, hitilafu baina ya mataifa mawili jirani ya Kiarabu na Kiafrika ya Morocco katu haziwezi kupatiwa ufumbuzi.
Aidha ameongeza kuuwa, hitilafu baina ya Algeria na Morocco zilipaswa kupatiwa ufumbuzi na pande mbili na haikupasa kuingizwa upande mwingine katika mzozo huo hususan utawala dhalimu wa Israel.
Algeria imekuwa ikimkosoa jirani yake Morocco na kumtuhumu kwamba, imeuingiza utawala wa Kizayuni wa Israel katika njama hatari dhidi ya serikali ya Algiers.
Tarehe 24 Agosti mwaka huu Algeria ilichukua hatua ya kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Morocco ikiituhumu Rabat kuwa imehusika na hatua kadhaa za kiuadui na kiuhasama dhidi yake.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria Ramtane Lamamra alitangaza kuwa, uamuzi huo hauwezi kubadilika, umechukuliwa kwa kuzingatia maslahi ya taifa na kwamba, Algeria imekuwa na subira muda mrefu kabla ya kuchukua uamuzi huo ikivumilia chokochoko za jirani yake Morocco.