Moscow: Utumaji wa silaha kwa nchi ya Ukraine ni sababu ya vifo vya raia wakawaida

Mjumbe wa Urusi katika Umoja wa Mataifa alisema Jumanne kwamba hatua ya baadhi ya nchi za magharibi ya kutuma silaha nchini Ukraine ni jambo litakalosababisha vifo vya raia wa kawaida waliopo mashariki mwa nchi hiyo.

Faraan: Imeripotiwa kwamba; “Mwakilishi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Bw. Gennady Kozmin, alisema wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hatua za baadhi ya nchi za Magharibi za utumaji wa silaha kwa nchi ya Ukraine na uwasilishaji wa washauri wa kijeshi zilihimiza Ukraine kuchukua hatua za uchochezi,”.

Aliongeza kuwa ; “Hii ina maana kwamba raia wanaendelea kuuawa mashariki mwa Ukraine, ikiwa ni pamoja na watoto, wazee na wanawake, na hii ni sehemu ya vita visivyojulikana vya Ukraine dhidi ya mikoa ya mashariki kwa miaka kadhaa,”.

Nchi za Magharibi, hasa Marekani, zimekuwa zikituma silaha hatari nchini Ukraine katika wiki za hivi karibuni.

Katika hali ambayo kwamba Maafisa wa Kiev na serikali ya Marekani na washirika wake wanadai kuwa kuwepo kwa wanajeshi wa Urusi karibu na mpaka wa Ukraine ni utangulizi wa mashambulizi dhidi ya nchi hiyo.

Urusi mara kwa mara imekua ikisema kuwa haina nia ya kuanzisha operesheni ya kijeshi dhidi ya Ukraine, na madai hayo hayana msingi wowote bali ni uzushi na uongo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *