MOSSAD imeua maafisa wake sita wa intelijensia kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na Iran

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umewaua maafisa wake sita muhimu kufuatia kufeli operesheni ya shirika lake la ujasusi Mossad ya kufanya hujuma na uharibifu kwenye kituo kimoja cha viwanda mkoani Esfahan nchini Iran.

Maajenti wa shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni Mossad walipanga kuripua kituo kimoja cha viwanda mkoani Esfahan, lakini walikamatwa na wizara ya intelijensia ya Iran kabla ya kutekeleza operesheni yao hiyo.
Mossad, ambayo ilihisi kufichuliwa kwa operesheni yake hiyo tata ya hujuma ni pigo na kashfa kubwa kwake, iliona kwa dhana yake, ili kuzuia kupenya vyombo vya usalama vya Iran ndani ya shirika hilo, haina budi kuwaangamiza maafisa hao wote ili pengine iweze kuwalinda maajenti wake wengine waliosalia na kuendeleza mawasiliano nao.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Tasnim, kufuatia operesheni tata ya usalama ya Mossad ya kutaka kuhujumu kituo kimoja cha viwanda cha Esfahan, iliyopelekea kukamatwa watekelezaji wake wote na wizara ya intelijensia ya Iran, mbali na kumtimua afisa wake anayehusika na kitengo cha Iran, shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni liliwaondoa pia maafisa wake sita muhimu wa kitengo hicho kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na vikosi vya usalama vya Iran na baadaye kuwaua kwa sura tofauti.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala wa Kizayuni umethibitisha kuuliwa watu hao sita wakati walipokuwa wakihojiwa na ambao majina yao ni Tomer Ixeg, Ayalon Shapira, Sharon Small, Shayli Westland, Ofek Aharon na Itamar Al-Harar.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, maafisa wengine kadhaa wa Kizayuni wameuliwa na kitengo cha kupambana na ujasusi cha Mossad kwa njia tofauti, ikiwa ni pamoja na matukio ya ajali ya gari, lakini idadi yao halisi na hatima hasa iliyowafika haijulikani
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *