Wizara inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru imetangaza kuwa Sheikh Khader Adnan, mfungwa Mpalestina amekata roho na kufa shahidi ndani ya gereza la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Sheria ya uwekaji kizuizini kiidara inatoa ruhusa kwa Wazayuni kumshikilia mtu kwa muda usiojulikana bila kumfungulia mashtaka. Kwa mujibu wa taasisi zinazofuatilia hali na matibabu ya wafungwa, wafungwa wapatao 500 kati ya takriban wafungwa 4,900 walioko kwenye magereza ya Israel wanashikiliwa kwa kutumia sheria hiyo.
Mahakama ya kijeshi ya utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel imekataa mara kadhaa kumwachia huru kwa dhamana Sheikh Khader Adnan ili akapatiwe huduma za matibabu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Iranpress, Wizara inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru imetangaza leo asubuhi kuwa Sheikh Adnan amekufa shahidi ndani ya seli aliyokuwa amewekwa katika jela za utawala wa Kizayuni baada ya siku 86 za kususia kula.