Msururu wa hukumu za vifo na kunyonga watu kwa halaiki; rekodi ya jinai aliyojiwekea Bin Salman

Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua kuwa viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 15 walioshtakiwa kwa masuala ya kiitikadi, na kwamba kwa kutolewa hukumu hizo, idadi ya watu walio hatarini kunyongwa nchini humo imefika 53, wanane miongoni mwao wakiwa ni vijana chipukizi na watoto wadogo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Saudi Leaks, shirika hilo limetahadharisha pia kuhusu mauaji ya halaiki ya makumi ya wafungwa, wakiwemo vijana chipukizi wanane, yaliyoamuliwa kutekelezwa na mamlaka za Saudia, na kubainisha kuwa idadi ya wafungwa walio hatarini kunyongwa ni kubwa zaidi kuliko majina yanayotangazwa na kwamba hakuna taarifa zozote kuhusiana na wafungwa wengine wengi.
Kabla ya hapo, Kamati ya Kutetea Haki za Binadamu Bara Arabu iliitaja Saudi Arabia “nchi ya hofu na unyongaji” na kutoa indhari kuhusu wimbi jipya la mauaji ya umati katika nchi hiyo hususan dhidi ya wafungwa wa kisiasa na wanaharakati wa haki za kiraia na haki za binadamu.
Kamati ya Kutetea Haki za Binadamu Bara Arabu ilieleza katika taarifa kwamba inafanya uchunguzi kuhusu hali mbaya na hatari ya kibinadamu na ya haki za binadamu inayotawala nchini Saudi Arabia baada ya kuongezeka hukumu za kifo zinazotolewa na Mahakama ya Jinai ya Riyadh dhidi ya raia wa nchi hiyo wakiwemo wafungwa wa kisiasa, wanaharakati na hata waandamanaji.
Kamati hiyo imeongeza kuwa, mahakama imetoa hukumu za kifo kwa kundi moja la raia kwa sababu tu ya kutumia haki yao ya kubainisha itikadi zao na kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii au kwa kushiriki maandamano ya amani ya kupigania uhuru wa binafsi, uadilifu na usawa wa kijamii.
Kamati ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Saudi Arabia imesisitiza kuwa, kuendelea kutolewa hukumu hizo za kiholela kunathibitisha uwongo wa madai ya utawala wa Saudia ya kuheshimu haki za binadamu na kufuta hukumu ya kifo.
Kamati hiyo vilevile imetangaza kuwa Youssef al-Manasif, Abdul-Majid al-Nimr, Jawad Qurairis, Fadhil al-Safwani, Ali al-Mabyuq, Muhammad al-Labad, Muhammad al-Faraj, Ahmad al-Idgham, Hassan Zaki Al-Faraj na Ali Al-Sabiti, wote wakiwa ni watoto wadogo ambao hawajatimiza umri wa kushtakiwa, wamejumuishwa kwenye kundi la watu waliohukumiwa kifo. Katika kurasa za wanaharakati wa vyombo vya habari, hivi sasa inavuma hashtag ya “Awqiful-Madhbaha” yenye maana ya “Simamisheni Uchinjaji”, ambayo imeanzishwa kutokana na kukaribia siku utawala wa Aal Saud umepanga kuwanyonga vijana hao.
Kwa muda mrefu na kabla ya kutekelezwa hukumu waliyopewa, watu wanaohukumiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia huwa wanakabiliwa na kila aina ya mateso ya kimwili na kiakili. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya, raia wa Saudia wanapata mateso ya kila aina kuanzia wanapokamatwa; na mateso hayo hayasitishwi kwa kutolewa hukumu dhidi yao, bali huwa wanaendelea kukabiliwa na miamala mibaya na miovu inayojumuisha pia watu wa familia zao.
Katika mateso ya kimwili wanayopata watu hao ni pamoja na kutiwa shoti za umeme, kukoseshwa usingizi, kupigwa na kutusiwa, kung’olewa kucha, kuning’inizwa miguu juu kichwa chini pamoja na aina nyinginezo za mateso, ambayo lengo lake ni  kumlazimisha mtu aliyeko kizuizini akiri au asaini hati ya kukiri kosa wakati wa hatua ya kuhojiwa. Miongoni mwa waliokabiliwa na aina hizo za mateso ni kijana chipukizi Mustafa Al-Darwish ambaye alinyongwa mnamo mwezi Juni 2021. Yeye alitishiwa kufunguliwa upya mashtaka na hivyo akalazimika kutia saini hati ya kukiri makosa.
Mara nyingi, mateso wanayopata watu huwasababishia ulemavu au maumivu ya kudumu, pamoja na kupoteza fahamu. Akthari ya wafungwa huwa wananyimwa haki ya kupatiwa matibabu.

Na jambo la nne ni kwamba, Saudi Arabia hutumia kwa wingi dola za mafuta kuziba midomo ya mashirika na kuzirubuni na kuzihonga nchi mbalimbali duniani. Ni kwa sababu hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilieleza katika ripoti liliyotoa Oktoba 2013 kwamba, viongozi wa Saudia wanaitumia turufu ya pesa kuizuia jumuiya ya kimataifa isikosoe wala kukemea hali ya haki za binadamu katika nchi hiyo.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *