Mtatiro aagiza mwalimu aliyezaa pacha wanne kuhamishiwa mjini

Tunduru. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuanza mchakato wa kumhamishia kwenye shule iliyoko mjini humo Mwalimu Judith Sichalwe mwenye miaka 29 ambaye amejifungua watoto wanne bila upasuaji katika hospitali ya Wamisionari ya Mbesa.

DC Mtatiro ametoa maelekezo hayo jana Juni 26 alipomtembelea Mwalimu huyo katika kijiji cha Mkapunda kilicho umbali wa kilomita 100 kutoka Tunduru Mjini ambako anafundisha.

Mtatiro ameeleza ni wajibu wa serikali ya wilaya hiyo kumrahisishia maisha mwalimu huyo ambaye anaweza kukabiliwa na hatari ya kushindwa kumudu gharama za maisha kutokana na idadi hiyo ya watoto wachanga kwa wakati mmoja.

Ofisa Tarafa Nalasi ambako mwalimu Judith anaishi, Salumu Kijumu ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuratibu misaada mbalimbali, lakini pia amewaomba Watanzania wote watakaoguswa na kazi ya malezi ya pacha hawa wanne kumsaidia mwalimu huyo.

DC Mtatiro ameomba Watanzania watakaoguswa kumsaidia Mwalimu Judith asisite kuwasiliana naye kupitia namba 0673 103 536 iliyosajiliwa kwa majina Judith Sichwale.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *