Mtu anayeafikiana na kila jambo hawezi kufuata amri za Mwenyezi Mungu

 

 Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

(Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)

 Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq

 Lahore – Pakistan

25th Nov. 2022

 

Hotuba ya 1: Tofauti kati ya Hifazat, Hisn, Taqwa na Ismat

Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika misingi ya Uchaji Mungu.  

Tambueni kuwa ucha Mungu ni mjumuiko wa mipango na mikakati kutoka kwa Mwenyezi Mungu yenye kumlinda mwanadamu na pasi na mwanadamu kuwa na Taqwa basi maisha yake yanakua hayana tofauti na yale ya mnyama.

Maisha ya mwanadamu bila ya Taqwa ni sawa na maisha ya wanyama na mfano wake ni maisha ya binadamu katika kizazi cha leo ambapo maadili ya binadamu yamepotea.

Mwenyezi Mungu ameiweka Taqwa katika kila jambo kwa ajili ya usalama wa jambo lile kulingana  na sehemu hiyo ya maisha. Mwanadamu analazimika kuunda jamii hivyo basi inamlazimu kuishi maisha ya kijamii.

Aina ya maisha ya kijamii ambayo mwanadamu anatakiwa kuishi yanawasilishwa na dini kwa unuani wa Hablullah (kamba ya Mwenyezi Mungu) ambayo unuani yake na moja kati ya vigezo vyake  ni Ummah.

Iwapo Mwanadamu ataiacha Hablullah basi ataishia kuunda jamii kwa misingi ya maslahi binafsi, uchu na matamanio, ataunda jamii ambayo itakuwa ni jamii inayonasibiana na maisha ya  wanyama.

Zipo jamii ambazo mhimili wake sio dini wala Hablullah, lakini badala yake zinakwenda kwa misingi ya matamanio na maslahi binafsi na ndio jambo lililowakusanya na kuwaleta pamoja. Misingi hii haitengezi mazingira ya kuimarisha msingi wa ubinadamu na badala yake huharibu.

Mwenyezi Mungu amemuamuru mwanadamu kufanya E’tesam na Hablullah ( kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu) na kabla ya haya, Mwenyezi Mungu anasema kwamba usiwe na Taqwa na hapo ndipo utaikaribia Hablullah.

Katika Surah Al-I’mran aya ya 102, Allah anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ ١٠٢

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu.

Waumini wameamrishwa kuwa na Taqwa ambayo itawahifadhi katika mauti na kutokana na Taqwa hii watafika mwisho na kufa wakiwa Waislamu.

Nimebainisha hapo awali kwamba katika Aya hizi kuna Taqwa na E’tesam pamoja na Allah, au kushikamana na Allah na E’tesam pamoja na Hablullah(kushikamana na Hablullah).

Taqwa na E’tesam zote zinabeba maana sawa na ulinzi. E’tesam maana yake ni kupata Ismat (kutokosea) na sio kushikamana au kung’ang’ania kitu ambayo sio tafsiri sahihi.

Kupitia Hablullah unahitaji kufanya maandalizi ya ulinzi. Hifazat na Hisn pia vilevile zina maana ya ulinzi katika Kiarabu, kama ambavyo Muhsinaat ina maana ya wanawake wema, safi na Hisn pia hutumika kwa maana ya ngome.

Lakini maneno haya yote yanamafungamano na ulinzi na hubeba sifa na maana tofauti za ulinzi.

Hifazat ina maana ya kulinda kitu kwa kukipa hifadhi. Kama ambavyo mchungaji wa wanyama anavyolichunga kundi ili lisitawanyike. Aina hii ya ulinzi ni Hifazat. Mambo fulani hupata ulinzi kwa kulindwa au kwa kua chini ya uchunguzi.

Hisn kulingana na pale Mohsinaat ilipotolewa unamaana ya ulinzi wa kipande fulani cha ardhi kwa namna ambayo kwamba hakiwezi kufikiwa. Kama ambavyo ngome inavyozungushwa kando ya nchi.

Lakini kama mtu anaweza kuingia katika nyumba au mahali basi yeye si Haseen. Kufanya kitu bila kupenyeza, kuvamiwa na kuingia kwa Kiarabu inajulikana kama Hisn.

Leo pia kama katika ngome za zamani zilikuwepo na mashirika mengi yamefanya mipango madhubuti karibu na pembezoni mwao ili kujilinda dhidi ya ugaidi.

Wale wanawake wanaowafanya wafikiwe na wanaume. Wanaume daima huwawinda wanawake bila kujali umri, na tamaa hiyo haina mwisho. Ni katika asili ya mwanaume kuwa na tamaa ya wanawake na kua na matamanio.

Wanawake nao vilevile wanapenda mali za mwanamume kama vile pesa, gari, matumizi ya kupita kiasi n.k. Wanawake wanahitaji ulinzi dhidi ya mbinu za mwanaume.

Ulinzi huu unaitwa Hisaan ambapo asiyekua mahram hawezi kumkaribia hata kwa macho au mikono. Hivi ndivyo inavyotakiwa inapofikia kwa wanawake.

Taqwa inayotoka kwa Waqaya ni ile kinga dhidi ya vitisho, hatari kutokana na  kitu kinachohatarisha maisha. Wiqaya ndio ngao ambayo ilitumika zamani katika vita.

Katika mfanano wa leo koti la kuzuia risasi au magari ni Wiqaya. Quran inaitaja Taqwa kama kinga dhidi ya mambo ambayo ni tishio la uharibifu kwa utu na  maadili ya mwanadamu.

Ismat pia ni jina la ulinzi, lakini ni aina ya ulinzi ambayo humlinda mtu kutokana na  uzinzi au uchafu wa aina yoyote.

Iwapo mwanadamu ataelekea kwenye uchafu basi kumzuia mwanadamu ni Ismat au kuzuia uchafu kumfikia mwanadamu vyote viwili vinachukua maana ya  Ismat.

Ismat ni kinga dhidi ya uchafu yaani Rijz, aina ile ya matamanio ambayo huishusha hadhi ya mwanadamu. Na hii hutokea kwa kumzuia mwanadamu kuifikia Rijz au kutoiruhusu Rijz kumfikia mwanadamu.

Kama vile kujizuia kuingia kwenye maji machafu au kusimamisha maji machafu kuwakaribia wanaume.

Katika Quran Taqwa inatumika kwa maana ya kumlinda mwanadamu na jamii kutokana na vitisho vyenye kuleta uharibifu. Na Taqwa hii inatakiwa isiwe ya kidhahiri na inapaswa itekelezwe kulingana na haki zake.

Ukitenda kwa uvivu basi tishio hilo mwishowe litakupata. Mazingira ambayo haya yamekuja yalihusiana na maisha ya kijamii ambapo amri kwa E’tesam imetolewa. Ismat hii inafaa ianzie kwa Hablullah yaani kupitia dini.

Nayo inategemea Taqwa yaani unapoweka msingi wako wa maisha kwenye Taqwa basi unaweza kufanikiwa kutimiza zoezi la E’tesam.

 

Hotuba ya 2: Mtu anayeafikiana na kila jambo hawezi kufuata amri za Mwenyezi Mungu

Taqwa ya kivitendo ambayo hufanya maisha ya mwanadamu kuwa salama inadhihiri katika msemo wa hekima na katika Sirat pia vilevile ipo.

Haina maana kwamba Sirat ya baadhi ya Maimamu na baadhi Mitume haikushimili jambo hili. Na kwa vile somo letu linahusiana na Nahjul Balagha tuchukue sehemu inayoangazia swala hili.

Maisha ya kila mwanadamu yanahitaji Taqwa ya kivitendo.

Katika hekima zake Amirul Mumineen kwa kusema no 110

وَ قَالَ عليه السلام: لَا يُقِيمُ أَمْرَ اللَّهِ سُبْحَانَهُ إِلَّا مَنْ لَا يُصَانِعُ وَ لَا يُضََرَّعْمَ َعَلَّا يُضَانَِمْ

Amri ya Mungu inaweza kutekelezwa tu na yule ambaye si mwadhinishaji (na mpokea rushwa), wala si mtiifu na kudhalilika (mbele ya wengine) wala kufuata uchoyo. 

Mambo haya matatu yakipatikana ndani ya mtu basi hawezi kamwe kukiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Tunaweza kuona wengi wameacha faradhi za Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu ameweka mipaka ndani ya Quran, Halali na Haram hizi zote ni Amr za Allah (s.w.t).

Na maadili pia vilevile ni Amr ya Mwenyezi Mungu na mfumo wa uongofu pia ni Amri ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka kwa ajili ya mwanadamu. Amri ya Allah vilevile ni utawala wa kiungu ambao pia hauwezi kuanzishwa na nafsi hizi tatu.

Musana’a, Mudara, Mudahna maana yake ni upole, ulaini au kuafiki. Mwenye kufanya maafikiano kamwe hawezi kusimamisha faradhi, amri na mfumo wa Mwenyezi Mungu.

Kwa msemo huu wa busara Amirul Momineen (a) ameeleza siri kubwa. Katika historia kwa nini utawala wa Kiislamu na mfumo wa Uimamu hausimamiwi kwa sababu unaimarika pale tu maafikiano dhidi ya mfumo wa Uimamu hayajafanyika.

Mudahna imefafanuliwa kwa kina katika mihadhara yetu ya Ita’at (utukufu). Katika Suratul Qalam;

  فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ

Basi usiwat´ii wanao kadhibisha.

 وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ

Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.

وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَهِينٍ

Wala usimt´ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,

هَمَّازٍ مَشَّاءٍ بِنَمِيمٍ

Mtapitapi, apitaye akifitini,

 مَنَّاعٍ لِلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ

Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,

 عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ

Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.

 أَنْ كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ

Ati kwa kuwa ana mali na watoto!

 

Washirikina wanataka kuafikiana na nyinyi, na kwa malipo yao wanataka muafikiane. Kisha sifa za Walid ibn Mughaira zimetajwa katika aya zilizotangulia na Mtume anaambiwa asikubali kuridhiana na mwenye tabia hizo.

Tumefundishwa kuafikiana na sio kubaki imara popote pale. Popote palipo na dhiki, ugumu unapaswa kufanya maelewano na hii ndiyo Sheria yetu mpya ambayo imeanzishwa kwa msingi huu.

Walid alikuja kwa Mtume ili kuonyesha upole na maelewano ili tuweze kuishi pamoja Makka. Mudahna linatokana na neno Duhn ambalo maana yake ni mafuta.

Kazi moja ya mafuta ni kufanya kitu kua laini. Kama ambavyo unavyotumia mafuta kwa masaji ili kulainisha misuli. Kama ambavyo leo tunatumia istilahi ya ‘kumtia mtu siagi’ ambayo ina maana ya kuwalainisha watu ambao wana msimamo mkali na dhabiti. Kuna watu wengi wana nguvu, wako imara lakini unapowapaka siagi wanalainika na kua wepesi wa kukubali.

Unapowabembeleza wanakua laini. Hivyo basi maana yake ni kumlainisha mtu kwa kuzungumza naye mambo ambayo kwayo yanaafikiana na misimamo yake. Maadui walikuja kwa Mtume (s) na pendekezo la mapatano. Leo hii mapatano haya yamekuwa ni sehemu ya dini na Mtume aliamrishwa asikubaliane na shirki na Kufr.

Hakuna maelewano katika jambo la Tauheed. Amirul Muminin (a) anasema Amri ya Mwenyezi Mungu inaweza kuanzishwa na mtu ambaye hafanyi Musana’a ambayo ina maana sawa na Mudahna.

Hii ina maana ya kupunguza msimamo wako kwa ajili ya kumnufaisha mtu. Kama ukiona siasa za Pakistani, Jeshi lililainishwa licha ya unyonge wote, viapo vilivyofanywa juu yao. Mkuu wa Jeshi mstaafu alitoa hotuba laini sana wakati wa kutoka.

Vilevile Kuhonga pia kunalainisha. Unatoa pesa ili kupata halali yako

Amirul Muminin (a) anasema kwamba asiyefanya Musana’a anaweza tu kusimamisha Amir ya Allah. Unaona tumekuwa tukifanya maelewano katika historia yote.

Wakiwepo kina Taghot, Banu Umayyah, Banu Abbas na Shais walimuunga mkono Banu Abbas kuunda serikali. Walipigana vita, na kufanya maandamano ya kuwadhoofisha Banu Umayyah ili wawaweke Banu Abbas madarakani. Haya yalikuwa maafikiano na kila mahali huu ndio ulikuwa msingi wa Amri ya Allah.

Hata sasa nchi haiongozwi na mfumo wa kimungu kwa sababu wamefanya mapatano na kila uovu na ufisadi. Tabia yetu ni kwamba tunaafikiana na kila kitu, kama ukandamizaji, mfumuko wa bei na matatizo yote.

Imamu Husein (a) hakufanya maafikiano, Mudahna, Musana’a kwa sababu Quran haikumruhusu. Imamu Husein (a) alisema siwezi kukubali kudhalilishwa kwa sababu Mola wangu hakubali.

Ikiwa akina mama wanawafundisha watoto wao kuafikiana na ufisadi, udhalilishaji, basi vipi atasimamisha Amri ya Mwenyezi Mungu na mfumo wa kiungu. Shinikizo ambalo Imam Khomeini (R.a) alilipata kutoka kwa sahaba wake mwenyewe.

Mahdi Bazargan Waziri Mkuu wa kwanza, Bani Sadr na wengine walikuwa wakifanya maelewano ya Imam lakini Imam alikataa katika tukio moja tu ambapo Imam alikubali kusimamisha vita na akasema kwamba ninakunywa kikombe cha sumu kufanya hivi sasa kuna mjadala nchini Iran kwamba ni nani aliyemlazimisha Imam kufanya hivi, ni nani aliyetengeneza mazingira kama haya?

Imam alimuuliza huyo Waziri Mkuu wakati huo kua bajeti yao  ni kiasi gani, akasema sifuri. Kamanda wa Sepah alisema hatuna silaha. Hali haikuwa mbaya lakini waliigiza kama sifuri kisha Imam akasema ninakunywa kikombe hiki cha sumu.

Wanaofanya Mudahna hufikia hatua hii.

Walikuja kwa Mtume kwamba hatutakususia, kukusumbua bali kufanya maafikiano madogo tu. Mwenyezi Mungu ameamrisha kuwa wanataka kufanya maafikiano, lakini nyinyi msifanye hivyo. Ukifanya hivi basi Amri ya Allah hataimarika.

Amirul Momineen (a) anasema mtu ambaye anafanya hivi hawezi kuanzisha Uimamu, kwa sababu aliweza kuwaona watu wa Kufa daima wakiwa tayari kufanya maelewano, walikuwa tayari kuuzwa kwenye vifaa vyovyote.

Mtu anaonyeshwa faida fulani na mwishowe anauzwa na kukubali kuuza taifa zima, dini na kila kitu chake. Mtu wa namna hii hawezi kusimamisha Amri ya Allah. Usimfanye mtu ambaye anafanya maelewano kuwa meneja, kiongozi na usitoe chochote mikononi mwa watu kama hao.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *