Mufti wa Masuni Iraq: Jinai dhidi ya makamanda wa muqawama inalazimu kulaaniwa Marekani

Mufti wa Waislamu wa madhehebu ya Kisuni nchini Iraq amelaani vikali jinai ya utawala wa Marekani ya kumuua shahidi Qassem Soleimani na Abu-Mahdi al-Mohandes na kueleza kuwa, jinai hiyo inalazimu Marekani kulaaniwa kila upande na kuchukuuliwa hatua.

 Sheikh Abdul-Mahdi al-Sumaidaie ameashiria jinai ya uwanja wa ndege iliyofanywa na Marekani na kubainisha kwamba, serikali ya Iraq inapaswa kuendeleza mashinikizo ya kisiasa na kisheria dhidi ya Marekani iliyohusika katika mauaji dhidi ya makamanda hao wa ushindi na hivyo kuhakikisha Washington inabeba dhima ya jinai yake hiyo.

Sheikh Amir al-Bayati, msemaji wa Mufti mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Suni nchini Iraq amebainisha kuwa, kilichofanywa na utawala wa Marekani chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump ilikuwa jinai na ukiukaji wa wazi kabisa wa mamlaka ya kujitawala Iraq.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020.

Ikulu ya White House na Pentagon zilitangaza kuwa Marekani ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *