Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 24 May, 2024
Hotuba ya 1: Mujahid ni yule anayetumia uwezo wote katika njia ya Mwenyezi Mungu
Hotuba ya 2: Mwisho wa Israeli umekaribia lakini pale tunaposimama
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35}
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka.
Taqwa sio hiari na baadhi ya watu wana uelewa mbaya juu ya hili. Quran imerekebisha uelewa mbaya wa kimakosa na dhana nyingi kama hizi kwa mwanadamu. Wengi wanaishi maisha ya kuridhika bila Taqwa kwa sababu ya kuendekeza kwa kiasi fulani matamanio, matamanio ya wanadamu yanatimizwa. Hatutambui kwamba hakuna sehemu yoyote ya maisha iliyo salama. Taqwa ni ulinzi ule ambao unamuepusha mwanadamu kutokana na vitisho angamizi na hatari zinazoweza kuleta uharibifu duniani na akhera. Kwa mpango huu wa ulinzi Mwenyezi Mungu amezungumzia hatua ya Taqwa katika Surah Maida aya ya 35.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35}
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka.
Aya ni yernye kutoa amri ya Taqwa na tumeshajadili kuhusu Waseela hadi sasa kwa sababu ya uelewa wa kimakosa kuhusiana na waseela na uelewa huu wa kimakosa umefikia kiasi cha kuweza kubadili maelekezo na kiini cha dini kunako kumuelekea Allah. Unaweza kuwapata baadhi ya watu wapo katika muhimili wa Allah lakini hautaipata jamii kama jamii wakiwa wanaenda pamoja na kwa namna moja. Katika Urdu na Kifarsi Waseela maana yake ni nyenzo na njia lakini katika lugha ya Kiarabu Waseela ni ukuruba ambao hupatikana kwa Rghba. Kwa sisi katika Kiurdu na Kifar4si Waseela ni wale watu ambao hutusaidia kutimiza matakwa yetu, kupata msamaha, n.k. kutoka kwa Allah. Kwa sisi mfumo wa Allah unaenda kwa kuwepo mtu kati kwa sababu tunafikiri kwamba hatuwezi kumuelekea na kumuomba Allah moja kwa moja ambapo kuna viumbe wengi wenye mahusiano na Allah pasina kuwepo nyenzo zozote. Imam Aliy (a) katika wosia wake kwa mwanaye Imam Hasan (a) anasema: usimfanye mtu yeyote kuwa na njia kati yako na Mwenyezi Mungu kwani atakuja kuwa kikwazo kwako. Kama vile haitakiwi kuwepo na mtu kati yeyote kati ya watoto na wazazi isipokuwa pale ambapo uhusiano wao utakuwa umevurugwa. Ikiwa njia au watu kati wataingia kati, watawatenga watoto mbali na wazazi wao. Wale ambao tumewafanya nyenzo na njia ya kumfikia Allah wao ni njia na nyenzo za uongofu. Elimu na kukua kwa mwanadamu hupatikana kwa njia hii tu ambapo Allah amewatuma Mitume, watakatifu wa Allah ili waweze kutuongoza kumuelekea Allah. Mwongozo una maana ya ishara zinazo onekana kwa uwazi ambazo hupambanua njia na hatima ya mwisho. Mitume ni wale ambao wana uwezo wa kunyonya ilimu ya Mwenyezi Mungu na kutoka katika nyoyo zao mwongozo huwafikia waumini. Haimaanishi kuwa wamesimama katikati na kwamba ubinadamu umesimama nyuma yao na Mwenyezi Mungu upande mwingine ambao hauwezi kufikiwa moja kwa moja. Leo kizazi cha wanadamu kimenaswa katika njia hizi. Kila mtu ana lengo la kufikia hatua fulani na baada ya hatua hiyo atafanya mengine yaliyobaki.
Ali (a) anasema kwa kadri uwezavyo usimfanye yeyote kuwa kikwazo baina yako na Allah. Kama sisi ni wageni kwa Allah basi hilo litatufanya kuwa mbali na kuhitaji kutafuta njia na nyenzo. Allah ana mafungamano na kila kiumbe ulimwenguni kama kiumbe, bwana na Mtoaji n.k. kazi ya mitume ni kuwaonyesha watu njia, kuwafanyisha mazoezi, adabu na vitendo ambavyo kwavyo wanaweza kupata ukuruba kwa Allah na sio kwamba wanawaambia watu kufungamana nao na kwamba wao ndio watashughulika na Allah. Kazi ya mitume, Maimam na Watakatifu wa Allah ni kumfanya kila mtu atafute ukaribu na Allah. katika kiola ibada nia tunayo iweka ni kupata ukuruba kwa Allah.
Ndani ya Aya hii tunatakiwa kutafuta, kufuata na kutaka ukuruba kwa Allah kwa Raghba. Tufanye Ibtighaa ambayo maana yake ni Baghya ambayo maana yake ni kuacha kila kitu na kuanza kufuatilia kitu kngine. Wabtaghu ilayhil Waseela maana yake ni kuacha kila kitu na kutafuta Raghba ambayo itakufikisha katika kwenye ukuruba wa Allah. Na Raghba huja pindi mtu anapoacha kila kitu na hufanya kazi hiyo tu. Lakini sisi hatuachi kila kitu na kufanya kitu kimoja basi tuyafanyayo sio kwa Raghba bali ni kutokana na ushawishi.
Nyenzo ambazo Allah alizituma kwa wanadamu kwa ajili ya kuwaongoza kwama Nbii ‘Isa, lakini watu waliwaweka katika nafasi ya Allah. Ndani ya Aya hii inaendelea ikisema Wajahidu fii sabeelih ina pambaneni katika njia yake Allah.
Jihad, Jihad maana yake ni kutumia nguvu zote, na rasilimal ulizopewa na Allah. Hii ni amri ya Allah, na jihadi maana yake ilihama na kutumika katika vita kitu ambacho katika akili ya kila mtu.
Vita ni moja ya marejeo ya Jihadi na sio maana ya jihadi. Neno Qital hutumika kwenye vita ambapo hupiganwa vita, ikiwa kuna kuuwa na kujitetea. Jihadi ina maana ya kutumia uwezo na uwezo wa aina mbili umeelezwa zaidi ndani ya Qur’an, kwanza ni jihad ya nafsi na ya pili ni jihadi ya mali. Jihadi ina maana ya kutumia uwezo wote ambao Mwanadamu. Inapokuwepo vita au uwanja wa mapambano wowote. Kila nyanja za maisha ambazo Allah kaweka sheria ni Sabilillah. Unaweza kuwa umetumia uwezo wako wote kwa ajili ya kazi fulani kwa muda. Hii sio jihadi kwa sababu jihadi inafanyika kwa nia na shauku. Kama unachoka kwa kusoma ukurasa mmoja au kwa kusikiliza mawaidha basi hii Bukhl na Bakhs ambazo maana yake ni kuacha kitu nyuma na kutopokea kila kitu. Mujahid ni yule anayetumia uwezo wake wote katika njia ya Allah. Wanaoweka kitu kwa ajili ya familia, watoto na kutoa 20% za Khums katika njia ya Allah. Mujahid sio yule anayetoa 20%, anatakiwa kutumia uwezo wake wote. Mtu mwenye kutoa muhadhara mmoja kwa siku sio Mujahid. Mujahid ni Ibrahim Raesi. Ambaye alitoa umri wa ujana wake wote na heshima zingine kwa ajili ya Allah. Raisi wa nchi ambaye anakufa mpakani maana yake ametoa kila kitu. Huu ndio uthibitisho na maana halisi ya kuwa ni watu tofauti kutoka katika makabila tofauti. Hawa ndio watu ambao hutimiza agano lao kama Qur’an inavyosema. Tazama ni kiasi gani Allah kakupa na umehifadhi kiasi gani. Usigawe kila ambacho Allah amekupa kwamba hiki ni kwa ajili ya watoto wangu na hiki ni kwa ajili ya Allah. Sema kwamba maisha yako, kifo chako na kila kitu ni cha Allah. Alichokupa Allah unaweza kugawana na akina nani? Ni akina nani ninaweza kuwaweka na Allah. Maisha yanatolewa kwa ajili ya Allah, lakini maisha hayo pia yametolewa na Allah. Ikiwa utaweza kurudisha kila kitu kwa Allah basi hapo unaweza kuingia katika wanaoitwa Mujahidina. Na wale ambao wamechukua kutoka kwa Allah na hawakurudisha basi hao wanaitwa Qaedina. Maisha, utajiri, watoto na heshima vyote hivi vinatoka kwa Allah hivyo virudishe kwake.
Shahidi Ibrahim Raesi ni mmoja wa Mujahidina ambao wapo kinyume na wote waliokuwa kwenye vyombo vya habari, nchi nyingine na hata maulama na wasomi walikuwa wakilenga mishale yao kuelekea kifua cha huyu mpambanaji. Hawa wanatokana na kabila la Amirul Mu’minina (a) pindi Ali (a) alipopigwa upanga alisema nimefaulu naapa kwa mola wa Ka’abah. Ibrahim Raesi ameenda kwenye faraja sasahivi. Siku ya kufa kwake kishahidi tazama matusi ambayo yalifanywa na watu. Hawa ni wapambanaji ambao Allah huwapa na wanarudisha na Allah hupokea na kukubali kutoka kwao pia kwa sababu Allah huchukua tena kutoka kwa Muttaqina (wachamungu). Tunawatazama watu hawa Rais na waziri wa mambo ya nje ambao walikuwa na vyeo na nafasi kubwa lakini hawakujiweka kama ulivyo utambulisho wao. Tafuta Taqwa, tafuta ukuruba ukiwa na Raghbat na tumia maisha yako yote katika njia ya Allah. Uwezo unaweza kuwa kitu chochote kama kuwa na sauti nzuri, hotuba, akili na kitu kingine chochote. Tumia hivi vyote katika njia ya Allah ili uweze kuupata ukuruba na ustawi.
Hotuba ya 2
Wale ambao wamekubali mpango wa Taqwa maisha yao ya duniani na akhera yapo salama. Leo hii kizazi cha wanadamu kimezoea kuishi bila ya kuwa na Taqwa na hasa Waislamu ambao walitakiwa kuwa viongozi, vigezo na watekelezaji wa Taqwa.
Walichukua fadhila, suhula, upendeleo wa dini lakini hawakutimiza matakwa ya dini. Imamu Husein (a) katika khutba ya Mina wanazuoni wanahutubiwa na kusema kwamba utu wako, heshima yako inatokana na Uislamu na leo hii mipaka yote ya Uislamu inavunjwa. Wanatakfiri wanasema kwamba ikiwa hatutamtetea Yazid basi hatutaweza kumtetea mtu mwingine yeyote kwa sababu ilitokana na kuungwa mkono na wasomi, wazee, wanazuoni ambao walikuwa msingi wa kumwingiza Yazid madarakani. Wanachuoni ambao Imam Husein (a) aliwahutubia walipata kila kitu kutoka kwenye Uislamu na dini hiyo ambayo imekupa kila kitu imepoteza kila kitu na hata huoni haya na kuishi dini ya kawaida.
Leo ni sawa na wakate huo ambapo Waislamu wanauawa kikatili lakini hakuna kinachotambuliwa na Umma wa Kiislamu. Nchi za Magharibi zinapendekeza suluhu ya mataifa mawili kwa ajili ya Palestina. Hii sio njia ya Waislamu. Leo nchi tatu zisizo za Kiislamu, Hispania, Norway, Ireland zimesema kwamba tuko tayari kuikubali Palestina kama taifa tofauti. Njia ya mashahidi hawa kama Raesi, Suleymani na mashahidi wa Palestina wana njia moja tu ambayo Israel inapaswa kuangamizwa na ni taifa la Palestina pekee linalopaswa kubaki. Kuikubali Palestina kama taifa maana yake ni kuifanya Israel ikubalike. Israel imeshindwa katika vita dhidi ya Hamas. Kuua watoto, kuharibu miji sio vita. Hati ya kumkamata Netanyahu inatolewa na mahakama ya kimataifa lakini Amerika inashinikiza kusitisha. Israeli haikuweza kufikia malengo yoyote ya vita na wanajua hata wataendelea kupigana kwa miaka 100 hawawezi kufanya hivyo kwa hivyo inawapasa kutafuta njia mbadala. Njia moja mbadala ni kumtaka Bin Salman kufanya utakaso wa Hamas na pili ni kukubali sehemu moja ndogo ya ardhi kama Palestina na kuiacha Israel ikubalike na mataifa mengine yote. Wanajaribu kufikia malengo ya vita yaliyoshindwa kufikiwa kwa kupitia mbinu zingine.
Hii ni akili ya kawaida mtu anapochukua njia chafu zaidi inamaanisha kuwa ameharibiwa. Kundi lolote linalotaka kukimbilia kwenye mapaja ya Yazid litaangamizwa lenyewe. Ikiwa Waarabu wanajaribu kuanzisha mamlaka yao, tawala chini ya mapaja ya Israeli na kama Pakistan inatafuta mikopo kutoka IMF ili kupata kimbilio, basi uchafu huu ndio ambao unapaswa kukomeshwa. Mko sawa mpaka mmefanya nchi za Kiislamu zilale usingizi na kuzigawa makundi makundi. Unapaswa kujua kuwa wito wa mwamko ulitolewa miaka 45 na Imam Khomeini (r.a) na Hamas ni mtoto wa mapinduzi. Uchafu huu wote unaenda kuharibiwa. Mauaji haya ya kishahidi ni uthibitisho tosha kwamba mwisho wao umekaribia. Jamii inayojifunza kufa hakuna anayeweza kuiangamiza. Unaona msafara wa mazishi katika miji mbalimbali ambapo mamilioni ya watu huhudhuria mazishi. Hudhurio hili la mazishi halikuwa jambo la kawaida bali ni ujumbe uliotolewa kuwa mtu akiuawa kishahidi basi milioni moja wako tayari kuuawa kishahidi. Wale walio chini ya kambi ya Wilaya hawakabiliwi na fedheha. Uchafu lazima uishe lakini tunapaswa kuchukua uamuzi wa pale tunaposimama. Isiwe kwamba sisi pia tunamalizika pamoja na uchafu. Kuna ukimya wa fedheha juu ya Palestina nchini Pakistan na hii haipaswi kutokea. Israel na dunia ziko chini ya shinikizo kubwa la sivyo wasingeikubali Palestina. Hamas wameweka mkono kwenye mshipa wao wa shingo ambao ungekatwa na hatupaswi kuona aibu wakati huo. Mwenye kuchukua jina la Husein na kisha kusimama katika safu za Yazid si Husein bali ni mchafu zaidi.