Muungano vamizi wa Saudia waendelea kukiuka usitishaji vita nchini Yemen

Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeendelea kukiuka makubaliano ya usitishaji viita ambapo katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita umekiuka usitishaji vita huo mara 202.

Usitishaji vita wa muda wa miezi miwili ulianza kutekelezwa Aprili mwaka huu na mwezi Juni mwaka huu Hans Grunberg, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen akatangaza kuwa, pande mbili zimeafikiana kuongeza kwa muda wa miezi miwili mingine makubaliano hayo kwa masharti yale yale ya awali.

Aidha pande mbili ziliafikiana juu ya kuongeza tena kwa muda wa miezi miwili mara muda huo utakapomalizika, hivyo hii ni mara ya tatu kwa usitishaji vita nchiini Yemen kuongezewa muda.

Pamoja na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia kuafiki makubaliano ya usitishaji vita lakini umekuwa ukiyakiuka mara kwa mara na hivyo kudhihirisha wazi kwamba, hauna nia ya dhati ya kutekeleza usitishaji vita nchini Yemen.

Saudi Arabia huku ikungwa mkono na Marekani na nchi nyingine kadhaa, Machi 25 mwaka 2015 zilianzisha hujuma na mashambulizi makubwa huko Yemen na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa baharini, angani na nchi kavu.

Vita hivyo vya kidhulma vya Saudia na waitifaki wake huko Yemen hadi sasa vimesababisha kuuliwa maelfu ya Wayemeni, kujeruhiwa makumi ya maelfu na kuwa wakimbizi mamilioni ya wengine.

Aidha asasi na jumuiya mbalimbali za misaada ya kibinadamu zimetahadharisha mara chungu nzima kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen na hata uwezekano wa kutokea maafa ya kibinadamu katika nchi hiyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *