Muungano vamizi wa Saudia wazuia meli ya nne iliyobeba shehena ya mafuta ya Yemen

Shirika la mafuta la Yemen limetangaza kuwa, muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeizuia meli ya nne iliyobeba shehena ya mafuta ya nchi hiyo.

Mbali na kuiba mamilioni ya mapipa ya mafuta kutoka Yemen, muungano wa kijeshi wa Saudia umeshadidisha hali mbaya ya uhaba wa mafuta na fueli katika nchi hiyo masikini na iliyoathiriwa na vita kwa kukwamisha uingiaji wa meli zilizobeba mafuta kwa ajili nchi hiyo.
Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Masirah, msemaji wa shirika la mafuta la Yemen, Essam Al-Mutawakkil, ametangaza kuwa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na Marekani umeikamata meli ya “Tiara” iliyokuwa na shehena ya mafuta ya dizeli karibu na bandari ya Hudaydah, licha ya kuwa na kibali cha Umoja wa Mataifa.
Al-Mutawakkil ameongeza kuwa: kwa mujibu wa masharti ya usitishaji vita, imekubaliwa kuwa hadi meli 54 zinazobeba shehena za mafuta zitaruhusiwa kuingia katika bandari za Yemen lakini tangu usitishaji huo wa mapigano ulipoanza kutekelezwa ni meli 33 tu ndizo zimeruhusiwa kuingia kwenye bandari za nchi hiyo.
Msemaji huyo wa shirika la mafuta la ameongeza kuwa: Umoja wa Mataifa haujachukua hatua yoyote chanya kukomesha uharamia huo wa muungano huo vamizi.
Saudi Arabia, kwa uungaji mkono wa Marekani, Muungano wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine kadhaa, ulianzisha hujuma za kijeshi dhidi ya Yemen tangu mwezi Machi mwaka 2015 na kuiwekea vikwazo nchi hiyo vya nchi kavu, baharini na angani.
Usitishaji vita nchini Yemen ulirefushwa kwa miezi miwili zaidi mnamo tarehe 2 ya mwezi huu wa Agosti, lakini muungano vamizi wa Saudia unaendelea kukataa kutekeleza vipengee na masharti ya usitishaji vita, uliokubaliwa kwa muktadha wa kupunguza mbinyo wa mzingiro wa pande zote waliowekewa watu wa Yemeni, kwa kukiuka mara kwa mara makubaliano hayo.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *