Muungano wa Februari 14: Utawala wa Aal Khalifa Bahrain umetengwa

Muungano wa Februari 14 ambayo ni harakati ya upinzani nchini Bahrain umetangaza kuwa, utawala wa Aal Khalifa umepoteza muungano na waitifajki wake na hiivi sasa uumetangwa kikamilifu.

Ibrahim al-Aradi, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kisiasa ya Muungano wa Februari 14 amesema kuwa, utawala wa Aal Khalifa umetengwa hasa baada ya kuvurugika muungano na waitifaki wake na kwamba, hilo linaonekana wazi katika mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar.

Kiongozi huyo mwandamizii wa Harakati ya Februari 14 amebainisha kuwa, kilele cha kutengwa Bahrain kilidhihirika wazi baada ya kutoalikwa nchi huyo katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya soka ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Aidha amesema, wananchi wa Bahrain wameendelea kufanya maandamano na kutangaza upinzani wao dhidi ya hatua ya utawala wa Aal Khalifa ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel unaofanya mauaji kila uchao dhidi ya Wapalestina.

Kadhalika Ibrahim al-Aradi, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kisiasa ya Muungano wa Februari 14 amewataka wananchi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kutoisahau kadhia ya Palestina na watambue kwamba, watawala wanaofuatiliia kufanya mapatano na Isarel kwa ajili ya kulinda maslahi yao wapo tayari kuwakandamiza watu ambao wanapinga mpango mchafu na wa kisaliti wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

Tangu Februari 14 mwaka 2011 Bahrain imekumbwa na vuguvugu la harakati za mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa huru, kutekelezwa uadilifu, kukomeshwa ubaguzi na kuingia madarakani serikali itakayochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *