Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan amesisitiza kuwa, jibu la nchi yake kwa Ethiopia kuhusu mauaji ya wanajeshi wa Sudan katika eneo la mpaka wa al-Fashqa litadhihiri kwenye medani ya vita. Kwa mujibu wa baadhi ya wanajeshi wa Sudan, mapigano makali yalizuka kati ya wanajeshi wa Sudan na Ethiopia kwenye mpakani mwa nchi hizo mbili siku ya Jumatatu asubuhi.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Urusi, Al-Youm Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan, alipotembelea vikosi vilivyoko katika vituo vya Al-Asra na Wad Kuli katika eneo la Al-Fashqah kwenye mpaka wa mashariki, alisema. “Jibu letu la kuuwawa kwa askari wetu katika eneo la Al-Fashqah litakua katika uwanja wa vita.”
Aidha Al-Burhan amesisitiza kuwa: Kamanda wa Vikosi vya Silaha vya Sudan inakusudia kuviunga mkono vikosi hivyo na kuvisaidia kutekeleza jukumu lao takatifu la kuilinda nchi na kwamba, kamwe irada ya Wanajeshi hao haitadhoofika na kwamba wataendelea kuipigania nchi yao na wapo tayari kuuwawa kwa ajili ya nchi yao.
Mkuu wa Baraza la Uongozi wa Mpito alikariri: “Damu za mashahidi wetu hazitasahaulika na majibu yetu yatakuwa ukweli utakaodhihiri duniani, na matukio yaliyotokea katika siku zilizopita katika eneo la Al-Asra kamwe hayatarudiwa tena, na hatutaruhusu uvukaji wa mipaka ya kimataifa au kufanyika kwa uvamizi mpya katika ardhi ya Sudan au kwa raia wa Sudan.
Vilevile alikutana na wakazi wa wilaya za Al-Asra na Wad Kuli na kuahidi kukamilisha miradi ya umeme na miundombinu ya barabara.
Wakati huo huo, miongoni mwa vyanzo vya kijeshi vya Sudan viliiambia tovuti ya Sudan Tribune kua Mapigano makali kati ya majeshi ya Sudan na Ethiopia katika baadhi ya maeneo ya Al-Quraysh na Basandeh yalizuka manamo siku ya Jumatatu asubuhi , maeneo hayo yaliyo kwenye mpaka wa pamoja kati ya nchi hizo mbili.”
Kwa mujibu wa habari hizo, jeshi la Sudan lilizuia mashambulizi yao katika eneo la Tin al-Laban, mashariki mwa al-Asra, baada ya wanamgambo wenye silaha kuivamia Sudan huku wakisaidiwa na vikosi vya jeshi la Ethiopia.
Hapo awali, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilisema katika kujibu shutuma za Khartoum kwamba iliwanyonga wanajeshi wake saba: “Matukio ya hivi majuzi kwenye mpaka huo ni ya uzushi na askari wa jeshi la Sudan wameuawa na wanamgambo wa asili.”