Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Mkuu wa Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 28 June, 2024
Hotuba ya 1: Mwanadamu ana Wilayat katika maisha yake yote bila mamlaka kwa mwanadamu kwa ajili ya kuteua Walii.
Hotuba ya 2: Vita katika hatua ya kuamua na majeshi matatu yenye nguvu rasmi katika vita.
Maisha ya kisiasa ya mwanadamu ni mwelekeo muhimu wa maisha ya kijamii ambayo hupanga maisha yote. Cheo cha maisha ya kisiasa yaliyotolewa na Mwenyezi Mungu ni Wilayat. Mwenyezi Mungu amemuwekea mwanadamu mifumo lakini mwanaadamu anajitengenezea mifumo yake dhidi ya hiyo kama vile mwanadamu kubadilisha malengo ya maisha dhidi ya yale aliyoyaweka Mwenyezi Mungu. Vile vile, dhidi ya Ilani ya Mwenyezi Mungu mwanadamu ametengeneza njia yake ya maisha kama ya mababu, kitamaduni n.k.
Vile vile, dhidi ya Wilayat mwanadamu ametengeneza mfumo wa kisiasa kutoka kwa MaTaghoots. Taghot inatokana na Tughyan ambayo inamaanisha kitu kinachovuka mipaka kama mawimbi ya maji kuwa na msukosuko. Mwanadamu anatakiwa kuishi maisha yake ndani ya mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu lakini wakati fulani mwanadamu huvuka mipaka hii kitendo ambacho huitwa na Quran kama Fisk, Fujoor, Isyaan na Tughyan. Ni vipimo tofauti vya kitendo kimoja cha kuvuka mipaka. Taghoot ni mtu ambaye amevuka mipaka katika kila nyanja ya maisha iwe ya mtu binafsi, kijamii, familia, kisiasa na kitu kingine chochote.
Dhidi ya Wilaya ya Mwenyezi Mungu ni Wilaya ya Taghoot ambayo ni ule mfumo uliowekwa kinyume na mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu. Yeyote anayefanya hivyo ni Taghoot. Wilaya ya Taghoot imeundwa na mwanadamu. Wilaya kama ilivyotajwa hapo awali haimaanishi urafiki ambao ni upotoshaji na hakuna mahali popote katika lugha ya Kiarabu Wilaya ina maana ya urafiki au hata msaada (Nusrat). Inawezekana kuwa Lawazim ambayo pia sio Bayyan. Nini maana ya neno Lawazim? Lazim ni kitu ambacho Malzoom inaunganishwa nacho na Mulazim ni muunganisho wa pande mbili kati ya hizo mbili. Lazim haimaanishi wajibu, ambayo ina maana ya kitu ambacho kimeunganishwa na kitu. Kama ilivyo kuwa kila kitu kilichounganishwa na ibada, chakula, maji ya kunywa ni lawazimu za haya. Kama chombo cha maji ni Lazim kwa maji.
Wilaya ina maana kwamba chombo kimoja kinatawala, kinazingira chombo cha pili kwa madhumuni ya kutimiza mahitaji fulani ya kitu cha pili. Kitu hiki kinachotawala kinajulikana kama Walya kwa Kiarabu. Urafiki maana yake ni kufahamu, kufahamiana na mtu fulani lakini haimaanishi kwamba rafiki mmoja anatawala maisha ya mwingine, anatimiza mahitaji muhimu au ana mamlaka juu ya mwingine. Urafiki ni mvuto unaotegemea uhusiano. Chombo cha pili katika Wilaya kiko chini ya udhibiti wa kitu cha kwanza. Watu fulani wanapotawala, hudhibiti mambo ya watu wengine hii ni Wilaya.
Katika jamii yetu na maisha yetu, tunaweza kuona kuna utawala na udhibiti wa wengine. Kama wakati mwingine mke anatawala mwanaume. Mwanamke huamua kwa ajili ya mwanamume kile anachopaswa kula, mahali anapopaswa kwenda na aina hii ya uhusiano ni Wilayat. Ikiwa mwanadamu anatawala kuliko hii hiyo ni Wilaya ya mwanadamu. Tunaweza kuona hata kwenye biashara ambapo tuna uhusiano mwepesi na wengine kwani wana kazi zao na zetu ni kama za wenyewe. Huu ni urafiki na sio Wilaya. Lakini ikiwa mtu anamtawala mwenzake katika biashara, basi hii ni Wilaya ya mwenye kutawala. Vile vile katika mambo ya kijamii ukiona chifu ana mamlaka juu ya kila mtu, anachukua uamuzi kwa ajili ya wengine; hii ni Wilaya. Ikiwa utatazama kwa karibu unaweza kuona upo chini ya udhibiti wa nani katika kila kitu. Ikumbukwe mikataba, ajira si Wilayat. Hata Walii anaweza kufanya mkataba na kumfanyia mtu kazi. Wilaya ni wakati sehemu fulani ya maisha yako au maisha yako yote iko chini ya udhibiti wa mtu fulani. Mwenyezi Mungu anasema huwezi kujipatia mwenyewe. Unahitaji mtunzaji maishani ambaye anaweza kukuongoza, kuchukua maamuzi kwa ajili yako lakini huwezi kujifanya Walii mwenyewe. Katika familia zetu watoto badala ya baba kuwa walii wamemfanya mjomba kama Walii. Mwenyezi Mungu amemfanya baba kuwa walii wa watoto ambao baba pia hawezi kuwahamisha katika wilaya hii na kumpa mtu mwingine. Isipokuwa ikiwa tu baba ni mjinga (Safihu) na hawezi kuelewa mambo ya kila siku, kimsingi hawezi kutambua faida na hasara ya watoto, basi Babu atakuwa Walii. Kama babu si Walii, basi Hakim e Shar’iy atakuwa Walii wao. Safihu hawezi kuwa Walii, ambaye hawezi kutambua jema na baya. Hawawezi hata kuwa Walii wa mali zao wenyewe pia.
Maisha ya mwanadamu ni kwamba anahitaji Walii ambayo inamaanisha lazima uishi chini ya mtu fulani na katika mfumo wa kisiasa ndio uwanja mkubwa zaidi wa hili. Walii ndiye anayesimamia (Tadbir) mambo ya watu. Tadbir kwa lugha ya Kiarabu maana yake ni siasa. Mwanadamu anahitaji Tadbir na Mwenyezi Mungu hana budi kuamua Tadbir kwa mwanadamu kama ilivyo kwa ulimwengu. Na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu amewapa wilayat Mitume, Watakatifu wa Mwenyezi Mungu.
Kosa moja katika Shia ni kwamba Wilaya ni ya Maasum tu na si kwa ajili ya mtu mwingine yeyote. Wilaya huanzia kwa Mwenyezi Mungu na kushuka ngazi za chini. Kama vile wewe ni Walii wa watoto lakini wewe si Maasumu. Adalat ni sharti kwa Wilayat lakini sio Umaasumu (Ismat). Uamuzi lazima uchukuliwe na Walii tu katika kusimamia mambo ya jamii. Kama baba aanavyokuwa ni Walii ikiwa ana busara na asiwe mjinga, na mama hawezi kuchukua maamuzi. Demokrasia, uchaguzi hauwezi kutoa Wilaya kwa mtu yeyote. Kama vile huwezi kufanya uchaguzi katika familia kubwa kuamua nani ni Walii. Kila baba ni Walii wa watoto wao.
Kama ilivyo katika mazishi tunasema nani ni Walii wa maiti kwa ajili ya kutoa ruhusa. Mtu anapokufa, huwa chini ya Walii wa mtu aliye hai. Maiti inawezekana akawa ameandika wosia wa mwisho kuhusu mazishi yake na ikiwa ni mzuri, unaweza kupokelewa kwa heshima, lakini kama ni upumbavu kama asemavyo hivyo na hivyo mtu asihudhurie sala yake ya mazishi basi huu wosia ni batili. Huu ndio utamaduni wetu kwamba hata baada ya kifo pia wilayat inaendelea. Katika urithi vile vile ni 1/3 tu ya mali ndio ana haki ya kurithiwa kulingana na wasia wa maiti na kinachosalia warithi wake ndio wanamua jinsi inavyopaswa kugawanywa. Bida’ah nyingine (uzushi) ni kwamba kabla ya kifo mirathi hugawanywa pale baba anapozeeka. Katika maisha yake anaweza kutoa chochote anachotaka kwa yeyote ambayo ni haki yake, lakini hakuna mtu anayeweza kumlazimisha kufanya ugawaji kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Wilaya inaendelea katika kila nyanja ya maisha na haki hizi zinatolewa na Mwenyezi Mungu. Nani Walii wa watoto, mali, maiti, hazina ya umma haya huamuliwa na Mwenyezi Mungu na walii ana mamlaka aliyopewa na Mwenyezi Mungu ya kuamua.
Urafiki umetoka wapi kuwa na maana ya Wilaya. Kama Mtume (s.a.w.w) atasema Ali ni Walii, basi mfanye rafiki, kama atasema msikubali Wilaya ya Mayahudi, basi msiwafanye Mayahudi kuwa marafiki? Huu ni upotoshaji, ujinga na upotofu. Wengine wameeneza upotofu huu kwa kutojua na wengine wamefanya kwa faida fulani.
Katika Surah Maida, Aya ya 57
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {57}
Enyi mlio amini! Msiwafanye marafiki wale walio ifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye kuamini.
Hapa wale wanaoikejeli dini yenu, Ahlul Kitabu na makafiri wasifanywe kuwa na Wilaya. Ikiwa una Taqwa basi Taqwa hapa ina maana kwamba hupaswi kumkubali mtu mwingine yeyote kuwa Walii wako isipokuwa wale walioandikiwa na Mwenyezi Mungu na hapa makundi matatu ambayo yamebainishwa kuwa ni yale yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu. Hapa tunatafsiri kwamba wasifanywe urafiki. Je kuna tatizo gani ikiwa Myahudi, Mkristo atakuwa ni rafiki ambaye hana mamlaka juu yako? Urafiki huo ni hatari ikiwa kila kitu chako kitakuwa chini ya udhibiti wao. Usiweke mambo yoyote ya kisiasa, kijamii ya waumini mikononi mwao. Unaweza kuwa na mahusiano nao mazuri isipokuwa kwa watu waliokatazwa kama wasiokuwa Mahram na kisha maadui, wapotovu wanaotenda maovu kwa uwazi. Usitoe udhibiti wa maisha yako kwa wengine lakini urafiki ni sawa. Je, tunasimama wapi ukilinganisha na Quran? Je, tuko karibu, mbali, juu, nyuma ya Quran? Angalia eneo lako na utaona umesimama dhidi ya Quran. Quran inasema waliamrishwa kumkana Taghot lakini wakamfanya Taghot kuwa Hakim (watawala).
Hapa Quran inasema msiwape haki, udhibiti wa jamii yenu kwa Taghot. Unachagua mamlaka kwa ajili ya uchaguzi wa Manispaa , kwa hivyo ni nani amekupa mamlaka. Na hiyo pia unachagua watu mafisadi. Unatoa haki, udhibiti wa miji yako kwa nani? Hao ndio Walii wenu. Unasema Ali ni Waliyyullah basi ni sehemu gani ya Lahore ina mamlaka na udhibiti wa Ali. Maagizo hayo yanaendeshwa na serikali, polisi, maafisa na kwamba pia mwanamke CM inamaanisha Wali mwanamke. Umewafanya kuwa Walii na Mwenyezi Mungu amekuzuia usijifanye Mawalii wewe mwenyewe. Usimamizi wa miji, taifa ni Wilaya.
Katika aya hii, rejea inafanywa kwa Ahlul Kitabu na Kuffar. Wanafunzi wa seminari hupata kitu cha kucheza kutokana na hili. Ukisema kwamba mtu yeyote ambaye hafanyi mzaha wa dini anaweza kuwa Walii, hili lingewachezesha wanafunzi wa dini na kuwachanganya. Hapa Mwenyezi Mungu hasemi kwamba ni wale tu kutoka kwa Ahlul Kitab wanaofanya dhihaka wasifanywe Walii. Ukiambiwa usile punda, basi dhihaka itakuwa tukisema tunaweza kula mbwa kwa sababu ni nyama ya punda tu ndio imekatazwa. Makatazo yaliyotangazwa wazi yanafanywa kwa yale mambo ambayo yamekuwa ya kawaida miongoni mwa watu. Kwa nini katazo hili linafanywa kwa Ahlul Kita na makafiri? Kwa sababu waumini wamewafanya kuwa Walii na kujihusisha katika maamuzi yao. Ikiwa makatazo hayafanywi kwa wengine, basi haimaanishi kwamba wanaweza kufanywa Walii………
Leo wale mliowapa kura na kuwafanya Walii si ndio wale watu wanaoidhihaki dini. Leo tunaweza kuona kile kichafu ambacho wanasiasa hawa wamefanya. Lau kama Aya hii ingeshuka basi makatazo yasingekuwa hasa kutoka kwa Ahlul Kitab, kwa sababu watu wa Pakistan hawajamfanya Ahlul Kitab kama Walii lakini hawa wasaliti wamefanywa kuwa Walii. Yeyote anayeifanya dini yako kama La’ab basi hawezi kufanywa Walii. Hii ni Taqwa ambayo inadai kwamba huwezi kumfanya Walii. Ikiwa huwezi kumfanya mtu yeyote kuwa Walii nyumbani kwako basi unawezaje kumfanya Walii katika jamii. Huna demokrasia nyumbani kwako, basi iweje umemchagua Wali katika jamii yako. Nani katika kizazi hiki anafanya mzaha wa dini anahitaji kuonekana kote.
HOTUBA YA PILI
Leo hii watu wanaona matukio ya moja kwa moja ya unyama kutoka Palestina lakini wako kimya. Hii ni kutokana na kuishi maisha ya kidini bila ya Taqwa. Lakini bado kuna baadhi ya watu wana dhamiri, ni wale walioshika msitari wa mbele na Hamas wamethibitisha kuwa hata likitokea kundi dogo la watu wenye Taqwa wanaweza kutawala na kulishinda kundi kubwa lenye nguvu ambalo limekiri kuwa haliwezi kuwashinda.
Miezi minane kabla watu walikuwa wanatazamia jambo ambalo sasa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu liko karibu kutokea. Hezbollah, Hashdu sisi Shabi na Ansarullah wanaingia vitani kivitendo na wamechukua ardhi kutoka kwa Hamas na kuwapa muda wa kuburudika na kujiweka sawa. Vikosi hivi vimeingia vitani rasmi kwa njia ya kimkakati na kufanya mashambulizi ya kupangwa. Hasara ni kubwa kiasi kwamba Israel imewahamisha watu kutoka mipaka ya Lebanon na Syria. Yemen inalenga meli zaidi sasa na Marekani, Uingereza wanafanya mashambulizi ya kieneo karibu kila siku kuvunja nguvu zao ili wasiweze kuwadhuru Israel. Kisha Hashdu Shaabi wameanza mashambulizi bila mapumziko yoyote. Hezbollah imesema iwapo Israel haitaacha unyama, basi tutaingia Israel ardhini na pia imetoa ramani ya eneo la kwanza watakalolichukua. Uhamiaji mkubwa kutoka eneo hilo umefanyika. Wamewasilisha kwa Israeli maandalizi fulani ambayo yamezua hofu kubwa na wasiwasi ndani ya Israeli. Siku chache nyuma mkutano mkubwa ulifanywa dhidi ya Netanyahu huko Israeli ili kusitisha vita. Jeshi la Israel linasitasita kupigana na mzozo kati ya serikali na vikosi umeanza. Chama cha upinzani kimeeleza nia ya kuiangusha serikali ya Netanyahu kwa kuunda muungano wa upinzani. Wanahofia kwamba ataimaliza Israel katika mchakato wa kuimaliza Hamas na mijadala yote hii inaendelea kwenye vyombo vya habari. Netanyahu ananufaika na uchaguzi ujao nchini Marekani. Mahakama ya kimataifa ya haki imeitangaza Israel kama mhalifu wa kivita.
Kutoka kwa vuguvugu la Hezbollah na washirika inaonekana kama vita vinaingia katika hali ya maamuzi. Mwandishi mmoja ameandika kwamba kama vita kati ya Hezbollah na Israel vitaanza basi hii itakuwa ni Armageddon ambayo ni vita vya mwisho. Balozi wa zamani wa Israel alitangaza kuwa nchi saba ziko tayari kupigana dhidi ya Israel ambazo ni Iran, Lebanon, Palestina Syria, Iraq, Yemen, Uturuki. Japo Uturuki ni kinyonga lakini wamesema vita hii ikianza basi tutasimama na Lebanon. Hali imebadilika ambapo Hamas hawako peke yao na pia bado wanaendelea kushambulia. Wanasema ikiwa Israel itashindwa na hawa basi hakuna anayeweza kulinda wafuasi na washirika wa Israel. Ahadi hii ingetekelezwa na Mwenyezi Mungu na tunaomba kwamba kizazi hiki kiweze kuona katika maisha haya. Sayyid Nasrallah. Tumewafunza vyema mashujaa 100,000+ wa Lebanon. Ikiwa kutakuwa na hitaji la kuongeza tutawapa wengine fursa. Hiki ndicho kiwango cha maandalizi na ni bora vita hivi viishie hivi kwa kuangamizwa kwa Israeli badala ya maazimio. Huu utakuwa ushindi kwa wale wanaopinga na kama muda utafika, basi vijana wa Pakistan Shia na Sunni watakuwa tayari kusaidia Hezbollah na Hamas ili kuiangamiza Israel.