Mwanahabari mtajika wa redio ya Somalia auawa katika shambulio la kigaidi

Kundi la kigaidi la al Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limehusika katika mlipuko wa bomu uliosababisha kifo cha mwandishi habari mtajika wa redio ya serikali ya Somalia huko Mogadishu.

Shambulio hilo limejiri jana katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kuilenga gari ya waandishi habari wa redio ya serikali.

Al Shabaab imekiri kuhusika na shambulio hilo la jana na kusema kuwa limefanya hivyo katika kulipiza kisasi kwa kumshambulia Abdiaziz Guled maarufu kwa jina la “Abdiaziz Afrika” Mkurugenzi wa redio ya serikali yenye makao yake huko Mogadishu.

Taarifa iliyorushwa na televisheni ya taifa ya Somalia imeeleza kuwa:” tumesikitishwa na kushtushwa na taarifa za kuuawa Mkurugenzi wa radio Muqdisho Abdiasis Afrika na kujeruhiwa Mkurugenzi wa televisheni ya taifa Sharmarke Warsame. Wawili hao walilengwa na shambulio hilo tajwa wakati wakielekea katika wilaya ya Shangani.

Shambulio la Mogadishu limejiri siku moja baada ya watu wanane kuuawa na wengine zaidi ya 13 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika mji wa Berdale katika jimbo la kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *