Mwandishi wa Kizayuni: Al-Sanuwar ameiacha “Israeli”

Mwandishi wa Kizayuni : “Yahya al-Sanwar anajua wazi kwamba yeye ndiye aliye juu katika vita hivi, kwa sababu kulingana na maoni yake, ushindi haumaanishi kulishinda jeshi la Israel, bali unamaanisha kufifisha mpango na mipango ya utawala wake dhidi ya harakati hii. ”

Kwa mujibu wa habari, mwandishi wa Israel “Jacky Khoji” katika makala katika gazeti la “Ma’ariu” alisema kuwa Yahya al-Sanwar, kiongozi wa makundi ya upinzani katika Ukanda wa Gaza, alipinga makubaliano yoyote ya kubadilishana wafungwa. kutuma misaada zaidi au siku chache za mapumziko au kuachiliwa kwa wafungwa wengi zaidi wa Kipalestina kwa ajili ya kuachiliwa huru mfungwa wa Israel, lakini baada ya miezi michache, ilidhihirika kuwa hii haikuwa tu hatua ya kimbinu bali pia ni mbinu ya kisiasa.

Mwandishi huyu alisisitiza kuwa mkakati wa Al-Sanwar sio kukurupuka na kutumia muda.

Ameongeza kuwa: Al-Sanuwar anajua kwamba yeye ndiye aliye juu katika vita hivi, kwa sababu kwa maoni yake, ushindi haumaanishi kulishinda jeshi la Israel, bali maana yake ni kufifisha mpango na mipango ya Israel dhidi ya harakati hii.

Mwandishi huyu Mzayuni alisisitiza: Inaonekana kwamba jukumu la Al-Sanuwar lilianzishwa tarehe 7 Oktoba (wakati wa operesheni ya kushtukiza ya Hamas dhidi ya utawala wa Kizayuni).

Khoji alisema kuwa sababu ya kutoachiliwa kwa wafungwa hao wa Israel ni mbinu za al-Sanwar na akaandika kwamba hiyo itakuwa ni kichocheo cha shinikizo dhidi ya baraza la mawaziri la Netanyahu na kwamba italishwa na familia za wafungwa hao.

Mwandishi huyu Mzayuni aliandika katika sehemu iliyobaki ya makala: Kuendelea hali hii na kutoachiliwa kwa wafungwa wa Israel kutapelekea kushadidi mashinikizo ya ndani na kuongezeka kwa mivutano na migawanyiko katika “Israel”.

Ujumbe wa Al-Sanuwar

Mwandishi wa makala hayo ameashiria jumbe tatu za Al-Sanwar kwa viongozi wa makundi ya Wapalestina walioko nje ya nchi na kusema: Katika ujumbe wa kwanza, Al-Sanwar amesisitiza kuwa, uongozi wa harakati hiyo kamwe hautakubali kusitishwa mapigano kwa muda. Kwa sababu lengo lao ni usitishaji vita wa kudumu na wa kina.

Ujumbe wa pili ni kwamba makundi ya Palestina yamepata mafanikio ya kustaajabisha ya kijeshi dhidi ya utawala unaoukalia kwa mabavu.

Katika ujumbe wa tatu, huku akikaribisha jaribio lolote la kusitisha mapigano, Al-Sanwar alisisitiza kuwa makundi ya Wapalestina yako tayari kukubali mpango au wazo lolote litakalosaidia kumaliza mzozo wa kijeshi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *