Nablos: Wapalestima 165 wajeruhiwa na wanajeshi wa Israel

Shirika la Hilal Nyekundu la Palestina limeripoti kuwa, Wapalestina wasiopungua 165 wamejeruiwa na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Nablos, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan jana Ijumaa pekee.

Kila siku Wazayuni wanaua na kujeruhiwa makumi ya Wapalestina pamoja na kuvunja nyumba zao, kuharibu mashamba yao na kuteka maeneo yao. Mamia ya Wapalestina wanatiwa mbaroni mara kwa mara na wanajeshi makatili wa Israel.

Shirika la habari la IRIB limelinukuu Shirika la Hilal Nyekundu la Palestina likisema kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamewafyatulia risasi Wapalestina na kujeruhi kwa uchache Wapalestina 165 katika kipindi cha siku moja jana Ijumaa.

Baada ya Sala ya Ijumaa ya jana, Wapalestina waliandamana kulalamikia jinai za Israel na walowezi wa Kizayuni. Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walitumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na Wapalestina wasio na silaha wala ulinzi.

Makundi ya wanamapambano wa Palestina hivi karibuni yalitoa tamko la pamoja na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Baitul Muqaddas na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Makundi hayo ya muqawama ya Palestina yalitoa onyo kali kwa Wazayuni na kusema kuwa, maafa yoyote yatakayotokea kutokana na jinai hizo, lawama zote zitakuwa ni za utawala wa Kizayuni.

Muda wote utawala wa Kizayuni unadharau sheria za kimataifa na msimamo wa jamii ya kimataifa wa kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi wanazoporwa Wapalestina.

Vitongoji vyote vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina ni haramu kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Nchi mbalimbali zikiwemo za Ulaya zimetangaza kususia bidhaa zinazozalishwa kwenye vitongoji hivyo haramu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *