Nakhaale: Shahidi Suleimani ni alikua kiongozi wa wanamgambo wa Palestina na mtetezi wa kadhia ya Palestina.

Ziyad Nakhaaleh, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina amesema katika maadhimisho ya mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Jenerali Haj Qassem Soleimani, Abu Mahdi al-Mohandes na masahaba wengine huko Beirut:Damu ya Shahidi Sulemani ilimwagika kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa kikwazo kikubwa kwa siasa za Marekani na utawala wa Kizayuni.
Aliongeza kuwa: Suleimani alikuwa mkuu wa wapiganaji wote wa Palestina na mtetezi wa kadhia ya Palestina.
Nakhaaleh amesema: “Makombora yaliyorushwa katika mji mkuu wa utawala wa Kizayuni yametufikia sisi chini ya usimamizi wa Qassem Soleimani.”
Naye Shahidi Soleimani alisisitiza kuwa ushindi hautawezekana bila mapambano
Aliongeza kuwa: “Wananchi wa Palestina na muqawama ndio wanaowaambia adui kwamba tutakuzingira hata kama una silaha zote duniani.”
Akaongeza kwa kusema kua: Kaumu inayosoma wito wa kuswali (adhana) na kusoma Qur’ani kamwe haitaanguka au kuangamia

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *