Gazeti la The New York Times limewanukuu maafisa watatu waandamizi wa utawala wa Kizayuni nakuripoti kuwa, katibu wa Halmashauri Kuu ya Hizbullah hakuwepo katika kikao cha makamanda wa Hizbullah wakati wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Dahiya.
Gazeti la New York Times likiwanukuu maafisa watatu waandamizi wa utawala wa Kizayuni limeripoti kuwa, Hashem Safiuddin, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Hizbullah ya Lebanon ambaye ana nafasi kubwa katika asasi za kisiasa na kijamii za muqawama wa Hizbullah, hakuwepo katika jengo hilo. inayolengwa na jeshi la Israel huko Dahiya.
Gazeti la The New York Times limeongeza kuwa, Hashem Safiuddin ni miongoni mwa shakhsia wachache waandamizi wa Hizbullah ambaye hakuwepo katika mkutano huo ambao ulishambuliwa na jeshi la Kizayuni na kupelekea kuuawa shahidi Seyed Hassan Nasrallah.
Gazeti la New York Times liliendelea kuandika, maafisa wa Israel wanaamini kwamba Hashem Safieddin hivi karibuni anaweza kutambulishwa na Hezbollah kama mrithi wa Seyed Hassan Nasrallah.