Ni nchi gani zimesitisha uuzaji wa silaha kwa Tel Aviv?

Uingereza imeingia katika orodha ya nchi ambazo zimesimamisha au kupunguza uuzaji wa silaha kwa utawala wa Kizayuni kutokana na vita vya Ghaza na wasiwasi wa kuzitumia kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu za kimataifa.

Uamuzi wa Uingereza wa kusimamisha uuzaji wa silaha kwa utawala wa Kizayuni ulifanywa baada ya kupitia upya leseni ya silaha iliyotolewa kwa Israel. Waziri wa mambo ya nje David Lammy alitoa ombi hilo muda mfupi baada ya kuingia madarakani mapema mwezi Julai.

Ingawa Uingereza inachangia sehemu ndogo tu ya mauzo ya silaha kwa Israel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikosoa uamuzi huo, akisema kuwa kwa kutumia au bila silaha za Uingereza, Israel itashinda vita hivyo na kuhifadhi mustakabali wetu wa pamoja. Wakati huo huo, Amnesty International ilielezea hatua hiyo kama “kidogo sana” na kutaka kusitishwa kabisa kwa uuzaji wa silaha.

Mbali na Uingereza, serikali za Italia, Uhispania, Uholanzi, Ubelgiji na Kanada pia zimesitisha au kupunguza uuzaji wa silaha kwa utawala wa Kizayuni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *