Nusu ya wananchi wa Saudia wanalalamikia ugumu wa maisha

Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, nusu ya wananchi wa Saudia Arabia wanalalamikia ugumu wa maisha na kupanda vibaya kwa bei za bidhaa.

Kwa mujibu wa al Khalij al Jadid, uchunguzi huo wa maoni umefanywa na shirika moja la kibiashara la eneo hili baada ya kuombwa kufanya hivyo na taasisi ya Marekani inayoitwa “Washington Institute.” Uchunguzi huo umefanyika baina ya tarehe 25 Julai hadi tarehe 15 Agosti 2022.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonesha kuwa, nusu ya raia wa Saudi Arabia wanalalamikia hali mbaya ya maisha. Malalamiko hayo yanaonekana kwa watu wote, watu wazima na vijana.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, malalamiko hayo yanatokana na mfumuko wa bei za bidhaa muhimu za chakula na sera za serikali ya nchi hiyo kutegemea mno pato la kuuza nje mafuta ghafi.

Hivi karibu Idara Kuu ya Takwimu ya Saudi Arabia ilitoa ripoti na kusema kuwa, wastani wa bei ya bidhaa za matumizi kwa raia wa nchi hiyo katika mwezi uliopita wa Julai imepanda kwa asilimia 2.7 ikilinganishwa na muda kama huo mwaka uliopita.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, wastani wa mfumuko wa bei nchini Saudia kwa mwezi uliopita wa Julai umeathiriwa na kupanda vibaya bei za vyakula na vinywaji, huku kupanda gharama za usafiri na uchukuzi kukihesabiwa kuwa moja ya sababu kuu za jambo hilo. “Mfumuko huo wa bei nchini Saudi Arabia haujawahi kuhushudiwa katika kipindi cha miezi 13 iliyopita,” imesema ripoti hiyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *