Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amelaani jinai iliyofanywa na baadhi ya wanachama wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali ya kuchoma moto nakala ya Qur’ani Tukufu huko Stockholm Sweden.
Rasmussen Paludan kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia kwa jina la “Stram Kurs” au ‘Msimamo Mkali’ jana alichoma moto nakala ya Qur’ani Tukufu karibu na ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm tena huku polisi wakiwa wameimarisha hali ya ulinzi na usalama. Kitendo hicho cha Paludan kimelaaniwa vikali na Waislamu na nchi za Kiislamu; ambapo serikali na Sweden imekosolewa kwa kushindwa kuzuia kitendo hicho cha kuwavunjia heshima Waislamu na matukufu yao.
Hussein Ibrahim Taha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC pia ametahadharisha kuwa kitendo hicho cha uchochezi ambacho kimetekelezwa mara kadhaa na wanachama wa mrengo wa kushotoa wenye misimamo ya kufurutu ada kimewalenga Waislamu na kuyavunjia heshima matukufu yao.
Katibu Mkuu wa OIC amesema, kuchomwa nakala hiyo ya Qur’ani kunadhihirisha chuki dhidi ya Waislamu na wageni na ameihimiza serikali ya Sweden kuwachukulia hatua zinazopasa wahusika wa hujuma hiyo. Katibu Mkuu wa OIC aidha ametaka kufanyika juhudi za kimataifa ili kuzuia kukaririwa tena kitendo kama hicho na kuungwa mkono mapambano dhidi ya chuki dhidi ya Waislamu na dini ya Kiislamu.
Wakati huo huo, Nasser Kan’ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kuendelea kutusiwa Qur’ani Tukufu katika nchi za Ulaya; ambapo mara hii kumeshuhudiwa huko Sweden, na kulaani vikali kitendo hicho