Gazeti la utawala wa Kizayuni wa Israel la Yediot Ahronot limeripoti kuwa, askari 14 wa jeshi la utawala huo wamejiua katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Moja ya tishio muhimu zaidi linaloukabili utawala haramu wa Israel ni katika sekta ya kikosi cha jeshi na kwamba, moja ya mapigo makubwa katika jeshi la Israel ni kuongezeka matatizo ya kisaikolojia miongoni mwa wanajeshi. Wataalamu wa Kizayuni wameeleza kuwa, ongezeko la idadi ya wanajeshi wa Kizayuni wanaojiua linaashiria ongezeko la mkanganyo wa kiakili na kinafsi miongoni mwa askari hao na kwamba, idadi ya wanajeshi wanaoomba kupatiwa ushauri nasaha wa kisaikolojia imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Kabla ya hapo, viongozi na vyombo vya habari vya Kizayuni wamekuwa wakizungumzia ongezeko la kutia wasiwasi mkubwa la askari wanaojiua katika jeshi la utawala huo na visa vingi vya makamanda na askari wanaume wanaowabaka askari wa kike katika vitengo mbalimbali vya jeshi hilo.
Duru za Kizayuni zimekiri kuwa, tatizo la kuchanganyikiwa limewakumba wanajeshi wa utawala haramu wa Israel na kubainisha kwamba, askari wa Kizayuni wanatoroka jeshini kutokana na hofu yao kwa wanamapambano wa Muqawama wa Palestina.
Ripoti za hivi karibuni kabisa zinaonyesha kuweko ongezeko kubwa la idadi ya wanajeshi wa jeshi la nchi kavu wanaoshiriki katika vikao vya ushauri nasaha na tiba ya matatizo ya kiakili na kisaikolojia pamoja na msongo wa mawazo. Wanajeshi wa Israel hukumbwa na wasiwasi na wahaka mkubwa pale wanapopatiwa habari ya kupelekwa vitani. Wanaona kupewa jukumu la kupelekwa vitani kwao ni sawa na kukabwa na jinamizi.
Tatizo jingine linaloukabili utawala huo kwa sasa katika sekta ya jeshi ni utoro uliokithiri na vijana kukweka kwenda kuhudumu jeshini.
Gazeti la Kizayuni la Maariv mwaka 2020 lilitoa ripoti na kutangaza kuwa, kiwango cha wanajeshi wa Israel wanaokwepa jukumu la kuhuduumu jeshini kutokana na matatizo ya kiakili na kisaikolojia imeongezeka kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake na kwamba, idadi ya askari hao imefikia 450 kutoka 350 mwaka 2019.
Gazeti hilo lilibainisha kuwa, jeshi la Israel limeshindwa kugundua sababu hasa za kuongezeka kwa kiwango kikubwa namna hii matatizo ya kiakili na kinafsi baina ya wanajeshi wake.
Takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa, jeshi la Israel linakabiliwa na hali ya kusambaratikka kikamilifu. Kwa mujibu wa utafiti mpya, akthari ya vijana katika ardhi za Palestina zilizopewa jina bandia la Israel wanafanya kila wawezalo kukwepa kwenda kutoa hudumu ya jeshi.
Huko Israel barua za maombi ya msamaha wa kitiba, kiakili na kidini ili kutokwenda kutoa huduma ya jeshi zimeongeza mno na kuzusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa maafisa wa jesghi la utawaala huo ghasibu. Takwimu zinaonyesha kuwa, takribani nusu ya watu wanaopatiwa barua za kusamehewa kutokwenda kutoa huduma ya jeshi hawana matatizo yoyote, bali lengo la kuomba barua hizo ni kukwepa kutoa huduma jeshini.