Ongezeko la wanajeshi wanaojiua lautia kiwewe utawala wa Kizayuni wa Israel

Gazeti la utawala wa Kizayuni wa Israel la Yediot Ahronot limeripoti kuwa askari 14 wa jeshi la utawala huo wamejiua ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu.

Wataalamu wa Kizayuni wameeleza kuwa, ongezeko la idadi ya wanajeshi wa Kizayuni wanaojiua linaashiria ongezeko la mkanganyo wa kiakili na kinafsi miongoni mwa askari hao na kwamba idadi ya wanajeshi wanaoomba kupatiwa ushauri nasaha wa kisaikolojia imeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot limeandika kuwa, kuna ongezeko la kutia wasiwasi mkubwa la idadi ya askari wanaojiua katika jeshi la Israel, ambapo katika mwaka huu wa 2022 pekee, wanajeshi 14 wamejiua, ikiwa ni idadi kubwa zaidi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

 

Kabla ya hapo, viongozi na vyombo vya habari vya Kizayuni wamekuwa wakizungumzia ongezeko la kutia wasiwasi mkubwa la askari wanaojiua katika jeshi la utawala huo na visa vingi vya makamanda na askari wanaume wanaowabaka askari wa kike katika vitengo mbalimbali vya jeshi hilo.
Moti Elmur, mtaalamu wa Kizayuni aliwahi kutanabahisha hapo kabla kwamba ongezeko la idadi ya wanajeshi wa Kizayuni wanaojiua ni kiashiria cha kukithiri hali ya mkanganyo wa kiakili na kinafsi miongoni mwa wanajeshi hao na kwamba idadi ya wanajeshi wanaoomba kupatiwa ushauri nasaha wa kisaikolojia imeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Duru za Kizayuni zimekiri kuwa tatizo la kuchanganyikiwa limewakumba wanajeshi wa utawala haramu wa Israel na kubainisha kwamba askari wa Kizayuni wanatoroka jeshini kutokana na hofu ya wanamapambano wa Muqawama wa Palestina…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *