Vyombo vya habari vya Qatar vimeitaja Palestina kuwa “mshindi wa mapema” wa Kombe la Dunia.
Palestina; “ingawaje Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar bado linaendelea, lakini tayari mshindi wa mapema ashapatikana” . Nchi hii imeiba mioyo na akili za mashabiki wa kandanda duniani.”
Haya ni maelezo ya Dima Khatib, mkurugenzi mtendaji wa Al Jazeera Plus, kuhusu uungwaji mkono wa mashabiki waliokuwepo kwenye Kombe la Dunia la Palestina.
Khatib aliandika kwenye tovuti ya mtandao wa Al Jazeera, ukitazama bendera zisizohesabika za Palestina, pamoja na kanga na sanda zilizopambwa kwa rangi za bendera ya nchi hii, utagundua kwamba vilio vya “Uhuru wa Palestina” ni vyenye kusikika.
Viwanja vya Qatar, sehemu wanazokaa mashabiki, mitaa, na pia kwenye mitandao ya kijamii.Utadhani kuwa Palestina ni miongoni mwa timu 32 katika michuano hii ya Kombe la Dunia.
Vilevile Vyombo vya habari vya Amerika Kusini vilivyopo nchini Qatar viliandika kwamba Palestina ni timu ya “thelathini na tatu” iliyokuwepo katika mchuano ya Kombe la Dunia.
Je, sababu ya vitendo hivi ni nini? Kombe la Dunia ni kubwa zaidi kuliko hafla ya michezo. Ni mkusanyiko mkubwa wa watu kutoka duniani kote kusherehekea mshikamano wa binadamu.
Mwaka huu, michuano ya Kombe la Dunia imefanyika katika nchi ya Kiarabu kwa mara ya kwanza, na imewaleta pamoja watu wa eneo hilo zaidi ya ilivyokua hapo awali.
Matokeo yake, Palestina imekuwa moja kwa moja kuwa mhusika mkuu wa hadithi na imewaunganisha watu wa nchi za Kiarabu karibu nayo.
Katika “sauti ya watu” ya nchi za Kiarabu, kuunga mkono Palestina kunaonekana kuwa kielelezo cha uhuru na ishara ya upinzani sio tu dhidi ya uvamizi bali pia dhidi ya serikali za Kiarabu.
Tuliona bendera kubwa ya Palestina katika michezo ya Kombe la Dunia, ikiwa ni pamoja na Tunisia na Ufaransa, na katika mchezo kati ya Morocco na Ureno, wachezaji wa Morocco walishika bendera ya Palestina katika pete yao ya kushangilia.
Hata mashabiki wa timu za Brazil na Uingereza walipiga kelele kwa ajili ya uhuru wa Palestina.
Vyombo vya habari vya Israel na raia waliruhusiwa kuja kwenye Kombe la Dunia kwa mujibu wa sheria ya FIFA, ingawa hakuna uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tel Aviv na Qatar.
Waisraeli wakoloni walifikiri kwamba michuano hii ilikuwa fursa ya kipekee ya kuonyesha kwa mara nyingine tena kwamba wana uwezo wa kushinda hali yao ya kutokubalika katika nchi za Kiarabu, lakini hali hiyo haikuwaendea vyema.
Mashabiki wa kandanda wamekataa kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari vya Israel. Video kadhaa zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba majaribio ya wanahabari wa Israel kuwahoji mashabiki wa soka kutoka Iran, Lebanon, Tunisia, Saudi Arabia, Qatar, Japan, Brazil, Yemen, Morocco, Misri, Jordan na Palestina yameshindwa.
Vyombo vya habari vya Israeli vinazungumza juu ya Waisraeli kuwa “vitu visivyofaa” nchini Qatar na mara tu watu wanapogundua kuwa wao ni Waisraeli, wanatupwa nje ya teksi na mikahawa hadi wanahabari wa Israeli wanalazimika kujitambulisha kuwa raia wa nchi zingine.
Mnamo 2020, Moroko, Bahrain, Sudan na UAE zilitangaza kuhalalisha uhusiano na Israeli, lakini tabia ya watu wa nchi hizi, haswa wachezaji wa timu ya kitaifa ya Morocco, ilionyesha kuwa hali hii ya kawaida ni kati ya serikali yao na Israeli. na nyoyo za watu ziko kwa Palestina.
Kusalimika kwa utawala wa kibaguzi wa Israel kunategemea tawala zisizo za kidemokrasia zisizosikiliza sauti za wananchi wakiwemo Wapalestina wanaotaka uhuru. Katika Kombe hili la Dunia, Wapalestina na washirika wao walifanikiwa kuisusia Israel.