Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuomba Palestina kupatiwa uanachama kamili wa umoja huo.
Novemba 29, mwaka 2012 Umoja wa Mataifa uliikubali Palestina kuwa mwanachama mtazamaji katika umoja huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu, Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amemwandikia barua Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambayo pamoja na mambo mengine imegusia matukio mapya na mabadiliko yaliyojiri karibuni na vilevile mikutano na mazungumzo aliyofanya na viongozi wa nchi mbalimbali.
Katika barua yake hiyo, Mahmoud Abbas ameashiria pia kwamba, kupatiwa Palestina haki ya uwanachama kamili na rasmi wa Umoja wa Mataifa, ni hatua kubwa mbele na yenye umuhimu kwa ajili ya kuwezesha kuundwa nchi huru ya Palestina.
Kwa zaidi ya miaka sabini sasa, haki za wananchi madhulumu wa Palestina zinaendelea kupondwa na kukanyagwa na utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel, utawala ambao kwa muda wa miaka yote hii umekuwa ukitenda jinai za kutisha na za kinyama dhidi ya Wapalestina.
Hujuma na mashambuluio ya askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina zimeshadidi katika wiki za karibuni, ambapo katika matukio mengi, askari hao wamekuwa wakiwalenga Wapalestina moja kwa moja kwa risasi moto