Poland: Nishati ya amani ya nyuklia ni haki ya kimsingi ya mataifa yote duniani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland ameyalaumu madola yaliyohodhi nguvu za nyuklia duniani na kusema kuwa, inabidi mataifa ya dunia yashirikiane pamoja kufaidika kwa njia za amani na nguvu za atomiki na kusitumiwe vikwazo kama njia ya kuyazuia baadhi ya mataifa kufaidika na haki yao hiyo.

Marekani iko mstari wa mbele kuziwekea vikwazo nchi nyingine hasa Iran ili kujaribu kuizuia isifaidike kwa njia za amani na nishati muhimu sana ya nyuklia. Muda wote Marekani imeiwekea Iran vikwazo vikubwa kama vya kiuchumi ambavyo wataalamu wa mambo wanasema havitokani na kitu kingine isipokuwa husda na chuki za dola hilo la kibeberu dhidi ya wananchi wa Iran.

Peter Szijjarto, Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland amesema katika mkutano wa kuangaliwa upya Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Atomiki (NPT) mjini New York Marekani kwamba, kuna wajibu wa kupatikana utulivu wa moyo kuwa, nishati ya atomiki haitumiwi isipokuwa kwa njia za amani; mataifa yote yanafaidika bila ya ubaguzi na nishati hiyo na vikwazo havitumiki kuyazuia mataifa mengine kustafidi na nguvu za atomiki kwa njia ya amani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland vile vile amesema kuhusu vita vya Ukraine kwamba nchi zinazotumia vibaya vita hivyo kutoa pigo baina ya magharibi na mashariki mwa Ulaya zinapaswa kuachana na mchezo wao wa jeopolitiki kwani ni kwa madhara ya Poland na nchi zote za mashariki mwa Ulaya.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *