Pop Francis: Tunayakubali mazungumzo ya kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Katika kujibu ujumbe wa Kiongozi huyo Muadhamu wa Mapinduzi, Pop Francis amesema yafuatayo; “Salamu kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na wale viongozi wa kidini wa Iran; Vile vile sisi tunayakubali yale  ayasemayo kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatollah A’rafi, mkurugenzi wa seminari hiyo, aliwasilisha ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa Pop Francis, ambaye ni kiongozi wa Wakristo wa Kikatoliki.

Katika kikao na Pop, mkurugenzi wa seminari zinazotoa mafunzo yakidini alisema: “Baada ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kujulishwa kuhusu ziara yangu, Amekusalimu na kuisifu historia yako na uhusiano wako na Amerika ya Kusini, vilevie alisifu na kusisitiza baadhi ya misimamo uliyochukua katika kulainisha na kuuweka sawa uhusiano kati ya Uislamu na Ukristo na kuwatetea wanyonge, ni matarajio yake kua utaendelea na utetezi wa wanyonge ulimwenguni, hasa Palestina na Yemen, jitahidi uwe na misimamo uliowazi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi anataraji kuwa, hatua zitachukuliwa kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa Palestina, na kwamba suluhu itatokana na kura za wananchi na uchaguzi baina ya Wapalestina miongoni mwao wafuasi wa dini zote za utawala wa Palestina.

Katika kuujibu ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa Ayatullah A’rafi alisema:Nifikishie salamu zangu kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mamlaka za kidini na wazee wa Iran; Vile vile tunakubali anachosema kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *