Putin: Marekani inapandisha bei ya nishati duniani

Rais wa Urusi ailaumu Marekani kwa kupanda kwa bei ya nishati duniani, akisema nchi zisizo rafiki hazitimizi makubaliano yao na Moscow.

Kulingana na Huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars.Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano alisema kuwa Marekani ndiyo ya kulaumiwa kwa kupanda kwa bei ya nishati ulimwenguni.

“Nchi zisizo rafiki zimeharibu mnyororo wa ugavi wa nishati hapa ulimwenguni katika upande wa kaskazini, na nchi zingine hazitimizi mikataba yao, na hii ni sababu ya moja wapo ya matatizo tunayokumbana nayo,” Putin alisema katika hotuba yake.

Kulingana na Sputnik Putin alisema; “Tuna uwezo wa kuuza nishati kwa nchi za nje zenye mahitaji makubwa,”. “Vilevile tunaweza kuongeza matumizi ya Russia ya mafuta, gesi na makaa ya mawe kwenye soko la ndani”.

Rais wa Urusi alisisitiza kuwa nchi yake ina mipango mikubwa ya kuimarisha na kupata mifumo ya urambazaji, na kusisitiza kuwa Marekani ndio yenye kusababisha ongezeko la bei ya rasilimali za nishati duniani.

Putin aliongeza kuwa hatua ya nchi za Magharibi kukataa kushirikiana kikawaida na Urusi, ikiwa ni pamoja na kwenye rasilimali za nishati, tayari imeziumiza nchi za Ulaya na Marekani.

Hapo awali, mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell alisema mkakati wa kupunguza utegemezi wa Russia kwenye rasilimali za nishati utachukua muda.

Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yameiwekea Moscow vikwazo vikubwa tangu kuanza kwa operesheni maalum ya kijeshi ya Urusi katika eneo la Denbas na kutaka kupunguza vikwazo vya uagizaji wa nishati kutoka Urusi ikiwemo mafuta na gesi.

“Kwa kulinganisha mapato ya gesi ya Urusi kutokana na bomba hilo, inaweza kuonekana kuwa mauzo ya nje yanaongezeka,” lilieleza chapisho la Marekani Paltico katika uchambuzi wa Ryan Heath, likisema kwamba Putin alikuwa akishinda vita vya kiuchumi vya Magharibi dhidi ya Urusi.Na kwa bei ya juu zaidi kuliko mwaka jana.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *