Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Mkuu wa Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 26 April, 2024
Hotuba ya1: Tawakkal sio jambo la Mwenyezi Mungu binafsi bali ni mfumo
Hotuba ya 2: Qatar imeonywa kuishinikiza Hamas kuwaachia huru mateka bila masharti
Mwenyezi Mungu ameiweka Taqwa kuwa ni mpango wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ulinzi wa maisha katika mfumo wa mwongozo. Moja ya mipango ya ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni katika hali ya ulinzi au kuzungukwa na maadui. Kwa waumini njia yake ni kwamba atakuwa na maadui kwa sababu hatakubali utiifu, kwa utawala wa mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kila mwanadamu anapokubali utiifu kwa baadhi ya Mataghuti huwa amekwenda kwenye njia ya maangamizo. Watu, watawala, Taghoot watafurahishwa lakini atakuwa amechagua njia ya uharibifu. Ukibaki kuwa ni muumini basi itabidi ukabiliane na uadui na hatari. Hapa vile vile Mwenyezi Mungu ameweka utaratibu kwa ajili ya waumini kubaki salama hasa pale waumini wanapokuwa ni wachache, nyenzo ni ndogo ukilinganisha na zile walizo nazo maadui. Katika hali hii vilevile, Mwenyezi Mungu ameweka utaratibu kwa ajili ya ulinzi na wokovu wao.
Katika Surah Maida, Aya ya 11, Mwenyezi Mungu anazungumza na waumini
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَنْ يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنْكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ {11}
Enyi mlio amini! kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, walipo dhamiria watu kukunyosheeni mikono yao, na akaizuia mikono yao kwenu, na mcheni Mwenyezi Mungu. na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.
Kuna amri mbili katika muktadha wa somo hili katika aya hii kwa waumini. Sio vita tu bali waumini kwa sababu yoyote ile wanaweza kuzingirwa na maadui. Kwa mfano, hali moja iko Gaza na nyingine iko India. Ndani ya Palestina kuna vita ambapo waumini wako macho lakini ni wachache kwa idadi, hawana silaha na hawana msaada wowote. Lakini nchini India hakuna vita na wala Waislamu hawako katika hali ya vita, makabiliano, upinzani lakini uchokozi uko katika sehemu zote mbili. Katika siku hizi ambapo ni mazingira ya uchaguzi uchokozi ni mkubwa kwa Waislamu. Katika sehemu zote mbili kuna utawala wa maadui dhidi ya Waislamu. Hapa tunaweza kuona kwamba Mwenyezi Mungu ameweka sheria kutoka kwenye Quran kwa hali zote mbili. Katika hali zote mbili kama Waislamu watazipitisha na kufanyia kazi sheria hizi mbili za Taqwa na Tawakkal basi Mwenyezi Mungu atadhibiti mikono ya maadui na Waislamu hawataangamizwa na maadui. Hii imehesabiwa kuwa ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba aliizuia mikono ya maadui. Mbinu ya ulinzi kupitia Taqwa ni tofauti kwa kila nyanja. Katika uwanja wa vita, upinzani una fomu tofauti na katika hali zisizo za vita hali inakuwa tofauti.
Taqwa ni kwa ajili ya kulinda maisha na Taqiyya ni ulinzi wa dini. Tunaweza kuona kama Waislamu watakuwa wamepata Taqwa. Tunaweza kuwaona Waislamu katika sala, ibada, Hajj, Umrah lakini haya hayawezi kuwazuia Israeli. Kufunga ni Taqwa lakini tunaweza kuona vita kadhaa vilipiganwa ndani ya Ramadhani kwa sababu Taqwa katika vita ina maana tofauti.
Jambo la pili ni Tawakkal ambayo ina maana kwamba waumini wanapaswa kuweka Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu. Kuna maana moja ya kawaida ya Tawakkul ambayo ipo katika akili za kila mtu na hii pia imetokana na masomo ya maadili na Usufi. Tunaelewa kuwa Tawakkal ni kama chochote ambacho hatuwezi kufanya, tunapaswa kumkabidhi Mwenyezi Mungu na kisha tuendelee kumtegemea Mwenyezi Mungu kufanya mambo ambayo tulipaswa kufanya wenyewe. Hii sio maana ya Qur’an bali inatoka katika nyanja za sayansi ya kiakili. Usufi wameingia kwa kina zaidi na kiroho zaidi lakini tafsiri zote mbili hazina maana ya Tawakkal. Katika fasihi Tawakkal maana yake ni kukabidhi kitu mikononi mwa wengine. Baadhi wengine wamezungumza juu ya vitu maalum kama vile unavyofanya hivi unapokuwa dhaifu. Sio kwamba unapokuwa dhaifu na hauwezi kufanya jambo hii maana haipo katika maana halisi na fasihi ya Tawakkal. Haya ni marekebisho yaliyofanywa na wanazuoni wa maadili na Usufi. Kwa mujibu wa maana ya Quran, uwe dhaifu au mwenye nguvu unatakiwa umkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yote madogo na makubwa. Lakini ili kumkabidhi Mwenyezi Mungu, tunapaswa kuufahamu mfumo wa Mwenyezi Mungu. Tunayo maeneo mengi ambayo Quran inayataja kuwa ni Sheria ambayo ni matendo yale ambayo yapo mbali na malengo yetu ya maisha. Mawazo yetu yamefungiwa na Sheria hizi na hivyo hayaendi kwenye maeneo ambayo yanapaswa kwenda.
Ulimwengu wa Mwenyezi Mungu unategemea mfumo. Kuna serikali fulani ambazo zina sheria lakini sehemu fulani kama Saudi hazina sheria bali Mfalme pekee. Tunafikiri Mwenyezi Mungu ni kama Mfalme wakati watu wanapo jidhihirisha Mwenyezi Mungu anachukua uamuzi mara moja na kutoa amri au kutunga sheria. Anawaamuru malaika kufanya jambo fulani au kutofanya kwa watu fulani wanaotafuta. Hii ni Shiriki na kila kitu kinachotegemea dhana hii ni upotofu. Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu na kisha kutengeneza mfumo wa ulimwengu mzima na kila kitu kimeumbwa na kuendeshwa kwa msingi wa mfumo. Mfumo huo hausimami popote. Kisha ndani ya ulimwengu Mwenyezi Mungu akaweka mfumo mwingine ambao ni Sharia. Mfumo wa kwanza ni wa viumbe vyote lakini kisha kuna sheria kwa wanadamu ambazo zinaitwa Sunan e Ilahi (desturi za kimungu). Kwa binadamu sheria zinazoitwa dini hizo ndio Sunan ya Mwenyezi Mungu. Kuna mfumo ambao kila mtu anaendesha mambo yake chini yake. Sio kwamba Mwenyezi Mungu kila siku hutoa maagizo mapya kulingana na kile ambacho watu wanafanya katika sehemu mbalimbali ya ulimwengu. Mwenyezi Mungu hawafuati viumbe na kusubiri wafanye kitu kisha ndio nione ni maagizo gani ninapaswa nitoe. Hili ndilo kosa la kimsingi ambapo Wanachuoni hawakuweza kulieleza kwa uwazi na hivyo kubaki mapengo ambayo kwayo tulitengeneza mawazo juu ya Mwenyezi Mungu.
Mfumo uliotengenezwa na Allah umepangwa kuwekwa sawa. Kuna vipimo mbali mbali vya maisha ya mwanadamu na mwenyezi Mungu ameweka mfumo kwa ajili ya hili. Ebu tuchukue mfano kutoka katika ulimwengu huu ili tuweze kuelewa mfumo huu. Kama katika ulimwengu wa viwanda tunajua ni namna gani vitu huzalishwa kupitia mfumo ambao sisi sote tunafahamu. Kwa mfano, tukitazama mfumo wa nguo, kwanza pamba hupandwa katika mfumo ambao itaweza kukua na kustawi. Kisha mfumo unaofuata huanza kwa kuitoa shambani na kuisafisha. Kisha mfumo wa tatu ni kuibadilisha na kuwa uzi na mfumo unaofuata ni kuifanya kuwa nguo na hapo hu8ingia katika matumizi ya mwanadamu. Tokea shambani hadi kufika kwenye matumizi ya mwanadamu hupita katika mifumo mbali mbali. Kuna mifumo mbali mbali ambayo ina mafungamano. Wakulima watafanya kazi yao vizuri na kisha kukabidhi pamba kwa mtu fulani kama watu wa viwanda. Watu wa viwanda watazalisha hatua yao na kumkabidhi kwenye mfumo wa tatu. Namna hii ikiwa utachukua ngano tokea shambani hadi kufikia kutumika kama chakula, kufungasha kusambaza na kisha kufikia kuwa tonge la chakula kuingiza mdomoni mwako. Mfumo mmoja hufanya kazi yake kama mkulima anayefanya kazi yake na kisha kukabidhi kwenye mfumo mwingine. Tawakkul ina maana hiki ulichokifanya kiwasilishe kwenye mfumo mwingine ambao ni wa vitendo vya kiulimwengu ambapo huwakabidhi watu wengine. Hii sio maana ya kiqur’an ya Tawakkul.
Tawakkul ina maana ya fanya sehemu yako na kisha kabidhi kwenye mifumo mingine. Mfano wa kidunia ambao nimeutoa ilikuwa ni kwa ajili ya kuandaa akili. Mifumo ya mwenyezi Mungu ipo kama hivi ambapo hatua fulani ya mfumo mwanadamu huhusika kama mfanyakazi ambapo kazi hukabidhiwa mwanadamu. Kama hufanyi nafasi hii je utakabidhi nini kwa wengine? Ni kama mtoto anapozaliwa hufikia wakati ukamkiabidhi shuleni, lakini je ikiwa mtu hajaoa? Kwa ajili ya kukabidhi kwa wengine unatakiwa kuwa na kitu cha kukabidhi kwenye hatua ifuatayo. Allah ametengeneza mfumo kwa mpangilio na tunatakiwa kujifunza dini kwa mpangilio huu. Tuna sheria ambazo hazifungamani na vitu, hivyo tunaiona dini kama haifai. Elimu ya dini sio ile kwamba unafahamu sheria bali unatakiwa kufahamu mifumo. Tunatakiwa kuifahamu dini, ulimwengu wa Allah kulingana na mfumo. Wanyama wao huzingatia ulimwengu kama lishe, lakini mwanasayansi anaweza kuona mfumo na kugundua mmoja baada ya mwingine. Dini pia ina matabaka ya mifumo na inatakiwa tuielewe dini kwa mpangilio huu. Suali lililopo leo hii ni kwamba ni nini faida ya dini katika ulimwengu huu kwa sababu mambo yanaendeshwa na mifumo. Tawakkul ina maana ya kuwa ni mfumo wa Allah baadhi ya sehemu hukabidhiwa mwanadamu. Naweza kutoa mfano wa IT; unaandika kitu kisha unakituma kwa mtu mwingine au kuprinti. Hii kutuma ndio maana ya Tawakkul. Mifumo ya Allah ipo hivi pia pale tu kunapokuwa na mafungamano. Inabidi utengeneze faili moja kisha ulitume, hii ni Tawakkul. Unakabidhi ulichokifanya kwa Allah na sio kukabidhi kile ambacho unatakiwa kukifanya mwenyewe kwa Allah pia. Kuna bedui mmoja alikuja kwa Mtume na kumuacha ng’amia wake nje ya msikiti bila ya kumfunga na ngamia akakimbia mbali. Mtume akamuuliza nini kimetokea, alisema nilimuacha ngamia nje kwa Tawakkul. Mtume alimuuliza je ulimfunga miguu huyo ngamia. Alisema hapana. Mtume alisema hii sio Tawakkul. Kumkabidhi mambo Allah haina maana kwamba unaandika barua na kuwakabidhi malaika waipeleke kwenye ofisi ya Allah, bali ina maana ya kukabidhi katika mfumo wa Allah. Ikiwa waumini watafahamu mfumo wa Allah na wakamkabidhi Allah kama wanavyokabidhi mizigo kwenye shirika la ndege hii ndio Tawakkul. Hukuwahi kuwaza kwenye akili yako kwamba unaweza kuibiwa. Lakini unafahamu katika akili yako kwamba huu ni mfumo kwa sababu shirika la ndege lina mfumo. Ni jambo la kawaida ulimwenguni. Leo hii makontaina ya bidhaa yanatoka China. Mtu hununua na kukabidhi kwa makampuni ya wasafirisha mizigo ambao huileta hadi kituo cha mwisho. Unamkabidhi kila kitu kwa kuamini, imani ambayo hukufanya huwaamini, kuwategemea na kuwakabidhi.
Allah anasema mimi ndiye Mola wenu mlezi nimetengeneza mfumo, ana kuna sehemu maalumu na hatua ambazo inabidi kuzitekeleza. Kwa hiyo fanya kazi yako na mkabidhi Allah na kuwa na imani. Unatakiwa kuamini, tegemea mfumo wa Allah. Waumini huamini shule kama nyumba ya bikon na kuwakabidhi watoto wao kwao na sio shule za kidini. Tawakkul ya Qur’an inawakilisha utegemezi kwenye mfumo wa Allah. Mfumo kamili wa jamii inabidi uwe kwa mujibu wa mpangilio uliotolewa na Allah na kisha ndio uweze kuwakabidhi watoto wako, na kila kitu kwenye mfumo wa Allah. Na yeyote mwenye kukabidhi mambo yake yote katika mfumo wa Allah hakuna kinachopotezwa. Leo Waislamu wamepotezwa kwa sababu wameacha mfumo wa Allah. Allah haruhusu kupotezwa sehemu yeyote ya maisha ya mwanadamu. Mwanadamu kama hukabidhi uwepo wake wote kwa Allah, hao basi ni mitume, Salihinam Siddiqeen. Unaitwa kwenda Hijja ili kufuata njia ya Ibrahim. Ikiwa tutaishi maisha yetu kama maisha ya Ibrahim na kisha zao litakuwa ni Ibrahim na Ismail. Kama utakabidhi mambo yako baada ya kufanya sehemu yako kwa Allah kama alivyofanya Ibrahim kisha Allah alimfanya kuwa ni mwenye kuheshimiwa na kuwa ni kigezo.
Hatuna tawakkul kwa sababu tuna wanafiki. Allah anasema kuwa baadhi hudai ya kuwa wao ni waumini lakini sio badala yake wanamdanganya Allah lakini hawadanganyi ila nafsi zao na hawatambui. Kama wewe ni muumini basi mtegemee Allah. Aya hii inahusiana na uwanja wa Jihadi ambapo tunatakiwa kupambana kwa upande wetu na kisha kumkabidhi Allah.
Hotuba ya 2
Bila ya kuwa na uchamungu ubinadamu hubadilika na kuwa unyama na kizazi cha sasa ni Ushahidi tosha juu ya hilo. Imethibitishwa kwamba watu hawa hawana dini na wala hawana utu. Hii ni kwa sababu hatuna Taqwa. Leo hii kuna wasomi wa hali ya juu, viongozi wa dini, wasomi, wafanye biashara na wadai wa kila kitu lakini kila mtu amefeli katika ubinadamu. Pindi ushenzi ulipoanza Gaza watu hawa wote bilioni 8 wamefunga macho yao. Pasina kuwa na Taqwa tunaweza kuona ni namna gani ubinadamu umetoweka leo hii.
Qatar, Misri, Saudi, Emirates ni maadui sawa na Israel na Amerika. Wamewanyakua Wapalestina. Kiongozi wa Hamas yupo Qatar na Amerika katika wiki imeiweka Qatar kudhibiti maafa katika eneo kwani ndicho kitovu cha uchochezi. Wametoa nafasi ya hifadhi kwa wakimbizi katika viongozi wa Hamas. Amerika imesema inabidi Qatar ilazimishe viongozi wa Hamas kuwaachia mateka huru kisha baada ya hapo ndio watazungumzia kusimamisha vita. Sasahivi Amerika amesema kuwaambia wote wawili kwamba hakikisha mateka wanaachiwa bila ya masharti la sivyo tutakata uhusiano wetu na nyinyi. Qatar sasa imesema kuwaambia viongozi wa Hamas kwamba sasahivi tunaacha jukumu la usuluhishi na imewaonya Hamas kwamba tutawatoa nchini kwetu kama hamtawaachia mateka. Watawakabidhi Israel au Misri. Haya yanakuja katika Habari. Huu ndio mkandamizo kwa Hamas lakini pia huu ni Ushahidi kwamba Israel wameshindwa katika vita hii japokuwa wameiharibu Gaza na kuuwa zaidi ya wanawake na Watoto laki moja 100000. Israel ilivamia Hospitali ya Shifa ikuwa kila mtu na kuwazika. Katika Hospitali moja waliwazika pia waliokuwa hai na picha zinatoka nje kila siku. Licha ya haya tabia ya aibu ya Waislamu inaonyesha kuwa ubinadamu umekufa yaani hakuna.
Hisia za kidini za madrasa za Pakistan zinaweza kuonekana kwamba ikiwa mwanamke atavaa na maandishi ya Kiarabu wako tayari kuungua lakini mapenzi yao hayakupanda kwa miezi saba. Wako mitaani kila siku kwa ajili ya kutetea dini. Lakini leo hii yote haya yanatokea, Quran pia imezikwa huko Palestina. Ubinafsi wa mwanadamu ni wa kifahari zaidi. Nchini Marekani wanafunzi wasio Waislamu wameweka kambi kwa ajili ya Palestina. Ni watu wa kawaida lakini ubinadamu wao haujafa ndani yao. Sauti yao ina nguvu na Amerika inawakandamiza. Na nchi yetu imejaa Madrasa ambao wapo tayari kukatwa vichwa lakini wako wapi sasa? Wanafunzi ambao wako huko kwa ajili ya masomo wamehatarisha masomo yao kwa ajili ya kuitetea Palestina. Unaweza kuona taasisi za kidini ambayo yako tayari kutoa changamoto kwa yeyote anayezungumza kuhusu Uislamu. Wasomi hawa ambao hata hawawezi kuona ubinadamu ukichinjwa lakini hawajali.
Amerika imepitisha kiasi cha bilioni 100 USD dola za kimarekani kupewa Ukraine, Taiwan na Israel. Je kuna yeyote ambaye amezidisha chuki dhidi ya Amerika. Mwanajeshi wa Amerika amejichoma moto na Waislamu wanaoishi Marekani na ulimwenguni kote wameonyesha huruma kupindukia. Hapa inabidi kuheshimu thamani iliyolala makaburini na sio kufa tukiwa na ufahamu. Kwa sababu ya watu kama hawa kuwa hai ndio maana adhabu ya Allah haiteremshwi. Wanapaswa kupaza sauti zao sana ili waweze kuwaamshwa hawa waliokufa na kuhamasisha wanaodhulumiwa. Kama tutaisahau Palestina na kufanya kitu kingine itakuwa ni dhambi. Namna gani hawa wasomi watamjibu Allah na namna gani watapata uokovu. Sidhani kama wana dalili yeyote ya kusamehewa kwa ukimya wao. Kama wataoa sauti na kutoa matamko naamini tatizo litatatuliwa lakini hawana ujasiri wa kufanya maamuzi. Familia nzima ya Ismail Haniya wameuliwa, Watoto wake wanne na wajukuu lakini hakuna aliyeona machozi kwenye macho yao. Mkwe wake alizungumza na kuwahutubia Waarabu katika mazishi akisema kwamba hatutaomba msaada kutoka kwenu kwa sababu mmefedheheshwa, mmedhalilishwa na mmekufa. Huu ni ukweli kwa kila Muislamu pia hasa mashia ambao wanabeba jina la Imam Husein.
Hisia za kidini za madrasa za Pakistan zinaweza kuonekana kwamba ikiwa mwanamke atavaa na maandishi ya Kiarabu wako tayari kuungua lakini mapenzi yao hayakupanda kwa miezi saba. Wako mitaani kila siku kwa ajili ya kutetea dini. Lakini leo hii yote yanatokea, Quran pia imezikwa huko Palestina. Ubinafsi wa mwanadamu ni wa kifahari zaidi. Nchini Marekani wanafunzi wasio Waislamu wameweka kambi kwa ajili ya Palestina. Ni watu wa kawaida lakini ubinadamu wao haujafa ndani yao. Sauti yao ina nguvu na Amerika inawakandamiza. Na nchi yetu imejaa Madrassa walio tayari kukatwa vichwa lakini wako wapi sasa? Wanafunzi ambao wako huko kwa masomo wamehatarisha masomo yao kwa Palestina. Unaweza kuona mashirika ya kidini ambayo yako tayari kutoa changamoto kwa yeyote anayezungumza kuhusu Uislamu. Wasomi hawa ambao hata hawawezi kuona ubinadamu ukichinjwa lakini hawajali. Jina la Imam Husein inabidi litokee popote palipo na mwenye kudhulumiwa. Popote palipo na Uyazid basi kuna uhusein pia. Mahusein ni wale ambao hukubali kuikabili hatari ya maisha na kusimama dhidi ya dhuluma. Maombolezo ya kweli ni kupaza sauti dhidi ya dhuluma. Sauti hii haipaswi kushindwa. Kwa damu ya mashahidi na watoto Mwenyezi Mungu atakomesha dhulma hii na kuiangamiza na kuifedhehesha Israel na washirika wao duniani na akhera.