Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imelaani vikali mpango wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel wa kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imelaani kuendelea njama za Israel za kuyayahudisha maeneo ya Quds na msikiti wa al-Aqswa na kubainisha kwamba, hatua hizo zinakwenda kinyume kabisa na hati ya Umoja wa Mataifa, misingi ya kimataifa, maazimio ya Umoja wa Mataifa na kukkiuka wazii kkabisa haki za taifa la Palestina.
Radiamali hiyo ya ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar inafuatia tangazo la Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala dhalimu wa Israel ambaye ametangaza baada ya kuunda serikali mpya kwamba, upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni moja ya ajenda kuu za serikali yake.
Utawala huo ulizikalia kwa mabavu ardhi za Palestina katika vita vya mwaka 1967; na azimio la Geneva linasema kuwa ni marufuku utawala wa Kizayuni kufanya shughuli zozote za ujenzi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala vamizii wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Mwezi Julai mwaka huu, Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena ulipitisha azimio linalosisitiza kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna haki ya kupora rasilimali za watu wa Palestina na za miinuko ya Golan ya Syria unayoikalia kwa mabavu.