Raia wa Zimbabwe wapiga kambi ubalozi wa Marekani kupinga vikwazo kwa miaka mitano sasa

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Zimbabwe wameendelea kupiga kambi mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Harare kupinga siasa za vikwazo za dola hilo la kiistikbari na wamesema kuwa, hawataondoka kwenye kambi hiyo madipale Marekani itakapofuta vikwazo vyake dhidi ya Zimbabwe.

Sally Ngoni, msemaji wa Muungano wa Broad Alliance Against Sanctions, ambao umepiga kambi mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Harare tangu mwezi Machi 2019 amesema: “Tumepiga kambi nje ya Ubalozi wa Marekani kwa karibu miaka mitano sasa, na tutaendelea kupiga kambi hapa hadi vikwazo vyote vitakapoondolewa tena bila ya masharti.”

Aidha amesema: “Kambi hii tuliyoianzisha mbele kabisa ya ubalozi (wa Marekani) ni ishara kwamba hali ya maisha ya watu wa Zimbabwe ni mbaya sana na imesababishwa zaidi ya vikwazo vya miongo miwili (vya Marekani) dhidi ya nchi yetu.

Wiki hii rais wa Marekani Joe Biden aliwawekea vikwazo watu 11 raia wa Zimbabwe, akiwemo Rais Emmerson Mnangagwa, kwa madai ya kuhusika na rushwa au ukiukaji wa kile kinachodaiwa na Washington kuwa ni haki za binadamu.

Mwaka jana wanaharakati hao wa Zimbabwe waliwasilisha kwa Mahakama Kuu mjini Harare kuitaka itoe amri kwa Marekani iwalipe fidia wananchi wa Zimbabwe kutokana na vikwazo vya miaka mingi ilivyowaekea.

Naye Rutendo Matinyarare, mwenyekiti wa harakati ya Zimbabwe Anti-Sanctions Movement ambalo nalo ni kundi linalopambana na vikwazo kwenye mahakama za kimataifa, alisema Jumatano kwamba vikwazo hivyo vya Marekani ni kinyume cha sheria.

Katika taarifa yake ya usiku wa kuamkia Alkhamisi, serikali ya Zimbabwe ililaani hatua ya Marekani ya kuiwekea nchi hiyo vikwazo vipya na kusisitiza kwamba, wanaoathiriwa na vikwazo hivyo ni wananchi wa Zimbabwe tofauti na madai ya uongo ya Marekani kuwa haiwalengi wananchi wa kawaida.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *