Rais Mwinyi ayakaribisha Madhehebu ya Bohora kuwekeza Zanzibar

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya mazungumzo na kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora (Dawoodi Bohoras) duniani, Syedna Muffaddil Saifuddin na kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa dhehebu hilo kuja kuekeza Zanzibar.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumapili Julai 3, 2022 Ikulu ya Zanzibar ambapo kiongozi huyo wa Madhehebu hayo akiwa ameambatana ujumbe wake ulionyesha azma ya kuendelea kumuunga mkono Rais Mwinyi katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Mwinyi alimueleza kiongozi huyo fursa mbalimbali zilizopo Zanzibar pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Zipo fursa nyingi Zanzibar, mnakaribishwa hakika Serikali imejipanga na mazingira yameboreshwa,”

Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na katika sekta ya utalii, uchumi wa bluu ambao unajumuisha matumizi na uendelezaji rasilimali za bahari.

Rais Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa dhehebu hilo kubwa duniani kuja kuekeza Zanzibar na kuwahakikishia kwamba Serikali imeweka mikakati madhubuti na ushirikiano mkubwa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *