Baada ya kukosekana kwa muda wa wiki 6 na kusababisha wasiwasi juu ya afya yake na mahali alipo, Rais Paul Biya wa Cameroon hatrimaye amerejea nchini.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 91 amewasili nchini kutokea Geneva, Uswisi, akiwa ameandamana na mkewe, Chantal Biya, na wala hakuzungumza na wananchi. Pamoja na hayo aliwapungia mkono wafuasi wake waliokusanyika karibu na gari lake lilipokuwa likiondoka kwenye uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde.
Maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha Cameroon (People’s Democratic Movement) walikuwa wamekusanyika barabarani kote kutoka uwanja wa ndege hadi ikulu ya rais huyo.
Baadhi ya watu kwenye umati huo, walikuwa wamebeba mabango ya kumkaribisha Rais, na kutoa salamu zao za heri.
Kutoweka rais huyo kutoka Cameroon kulizua uvumi ulioenea kwamba alikuwa mgonjwa mahututi
Lakini maafisa wa nchi hiyo walitoa taarifa wakisisitiza kuwa alikuwa mzima wa afya, na kusisitiza kuwa usalama wake lilikuwa suala la usalama wa taifa.