Rais Samia: Mikutano ya hadhara ya kisiasa sasa ruhsa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania leo Jumanne, Januari 3, 2022 amekutana na viongozi wa vyama 19 venye usajili kamili wa siasa nchini humo Ikulu jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara nchini humo lakini kuna wajibu wa kila mmoja na upande wa Serikali kuhakikisha mikutano hiyo inafanyika salama.

Akihutubia mjumuiko huo, Rais Samia amesema, ni wajibu wa vyama vya siasa ni kufuata kanuni na sheria zinavyosema huku akivitaka vyma hivyo vya siasa za kiustaarabu, kiungwana na bila ya matusi. Amesema ndani ya Chama chake Tawala cha CCM wanaamini katika kukosolewa na kujikosoa, kama ambavyo anaamini pia kwamba akikosolewa na kufanyia kazi changamoto ataendelea kuwa Rais. Aidha, amesema yeye haviiti vyama tofauti na CCM kama ‘Vyama vya Upinzani’ bali anaviita ‘Vyama vya Kumuonesha Changamoto’ kwani haaminini kama Watanzania wanapingana.

Katika kikao hicho kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, kila chama kimewakilishwa na watu wanne, mwenyekiti, makamu wenyeviti wawili wa Bara na Zanzibar pamoja na katibu mkuu. Miongoni mwa viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe. Mawaziri na viongozi mbalimbali wa Serikali nao wameshiriki kwenye mazungumzo hayo wakiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Wengine walioshiriki kwenye kikao hicho ni viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Mikutano ya hadhara ya kisiasa ilipigwa marufuku nchini Tanzania wakati wa urais wa Dk John Pombe Magufuli, hatua ambayo ililalamikiwa sana ndani na nje ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *