Rais wa Algeria amesisitiza udharura wa nchi za Kiarabu kushirikiana kwa ajili ya kusaidia mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala vamizi na ghasibu wa Israel.
Faraan: Abdelmadjid Tebboune ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas aliyeko safari nchini Algeria ambako ametangaza msaada wa Algiers wa dola milioni mia moja kwa taifa la Palestina.
Abdelmadjid Tebboune amefichua nia ya nchi yake ya kuandaa mkutano wa makundi yote ya Wapalestina hivi karibuni na ametoa nafasi mia tatu za masomo kwa wanafunzi wa Palestina katika vyuo vikuu vya Algeria.
Algeria imekuwa mstari wa mbele katika miezi ya hivi karibuni kupinga sera na siasa za utawala ghasibu wa Israel na ukandaizaji wake dhidi ya wananchi wa Palestina.
Misimamo hiyo ya Algeria imeshuhudiwa zaidi baada ya jirani yake, Morocco, kutia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na hivi karibunivilevile kutia saini hatia ya kuanzisha ushirikiano wa kijeshi na utawala huo ghasibu.
Algeria pia imekuwa mstari wa mbele kati ya nchi za Afrika katika kupinga suala la utawala haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika, AU.