Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo na Wairani wanaoshi Qatar kuwa ipo azma thabiti ya kupanua uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Iran na Qatar.
Rais Sayyid Ebrahim Rais wa Iran jana usiku alikutana na Wairani wanaoishi Qatar na huku akibainisha kwamba maingiliano ya watu wa nchi za eneo hili chimbuko lake liko katika itikadi, imani na utamaduni wao wa pamoja na kueleza kuwa, ustaarabu unaoshuhudiwa kwa jina la dini katika eneo ni utajiri adhimu ambao siku zote unapasa kufikiriwa kuimarishwa na kutoruhusu kushambuliwa na kupuuzwa katika zama hizi za mawasiliano ya kidijitali.
Rais wa Iran ameongeza kuwa: Wairani wanaoishi nje ya nchi pia wana haki sawa kabisa na raia wengine ndani ya Iran na kwamba serikali ina jukumu na masuulia ya kuwahudumia raia hao.
Rais Ebrahim Raisi aidha ameeleza kuwa: Wairani wanaoishi nje ya nchi wanapasa kurahisishiwa zaidi mazingira ya kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kuwekeza nchini. Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa licha ya azma ya maadui katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuweikea nchi hii vikwazo vikali.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alielekea Doha, mji mkuu wa Qatar kufuatia mwaliko rasmi wa Amir wa nchi hiyo Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Nchi Zinaouza Nje kwa wingi Gesi uliopangwa kufanyika leo.