Raisi: Iran daima inaunga mkono taifa lenye umoja na serikali yenye nguvu huko Iraq

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo kati yake na Waziri Mkuu wa Iraq hapa Tehran kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote inakaribisha na kuunga mkono taifa lenye mshikamano na serikali yenye nguvu huko Iraq.

Mohammed Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq jana Jumanne aliwasili Tehran akiongoza ujumbe wa kisiasa na kiuchumi wa nchi yake kwa shabaha ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika mazungumzo hayo, Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema amefurahishwa na uthabiti wa kisiasa na kuundwa serikali mpya huko Iraq na kusema: uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq ni uhusiano wa iana yake na mwema. Amesema: kuimarisha na kukuza uhusiano wa pande mbili kunapasa kupelekea kuboreka kiwango cha maingiliano na ushiriiano wa kikanda na kimataifa ili kurejesha zaidi amani na uthabiti katika eneo na duniani kwa ujumla.

Raisi aidha amesisitiza juu ya azma ya ran ya kupanua ushirikiano na kustawisha kiwango cha uhusiano wake na Iran katika nyanja za kiuchumi, kibiashara, kisiasa, kiutamaduni na kiusalama na kuongeza kuwa: Iran inataka kustawisha mabadilishano kati yake na Iraq katika nyanja mbalimbali za kibiashara na katika sekta ya nishati pia. Amesema, kufanyika mikutano ya mara kwa mara ya kamisheni za pamoja za ushirikiano kati ya nchi mbili kunaweza kuwa na nafasi athirifu katika kufikiwa lengo hili tajwa.

Kwa upande wake, Mohammed Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq amesema katika mazungumzo hayo na Rais wa Iran akiwa ziarani hapa Tehran kwamba: amefurahishwa na ziara yake hii hapa Tehran baada ya kuundwa serikali mpya huko Iraq na kueleza kuwa: Iran ina nafasi ya juu na bora katika uga wa uhusiano wa kigeni wa Iraq, na uhusiano kati ya nchi hizo mbili unazidi kupanuka kwa njia nzuri na ya kuridhisha.

Waziri Mkuu wa Iraq ameongeza kuwa, kuboreshwa kamisheni za pamoja za ushirikiano kati ya Iran na Iraq kumekuwa na taathira katika kuimarka ushirikiano na uhusiano kati ya Baghdad na Tehran; na kuna udharura wa kufanyika mikutano endelevu na mara kwa mara kati ya pande mbili hizo.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *