Raisi: Jina la shahid Soleimani ni nembo ya mapambano dhidi ya ugaidi duniani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika sherehe za kuadhimisha mwaka wa tatu wa tangu kuanza kurusha matangazo yake redio ya muqawama kwamba, leo hii jina la shahid Soleimani ni nembo ya muqawama na kusimama kidete katika kupambana na ugaidi ulimwenguni.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) aliuliwa shahidi kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani, tarehe 3 Januari 2020 akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq, mjini Baghdad.

Shahid Soleimani aliuawa shahidi pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu wa Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi wakiwa pamoja na wanamapambano wenzao wanane. Rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump ndiye aliyetoa amri ya kufanyika shambulio hilo la kigaidi dhidi ya wanamapambano hao 10 wa Kiislamu.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisema hayo katika ujumbe wake wa video kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa tatu wa kufunguliwa redio ya muqawama kwa ajili ya kuibakisha hai siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kusisitiza kuwa, shakhsia ya shahidi Soleimani inabidi kutambuliwa kwa jina la chuo cha muqawama.

Rais Raisi pia amesema, redio ya muqawama imeasisiwa kwa ajili ya kutangaza na kubainisha maana ya muqawama, kuwaelewesha watu kuhusu jambo hilo na kuwaandaa watu wote wakiwemo wananchi wa Iran na vijana wa eneo hili na mataifa mengine ya wanyonge duniani kuhusu umuhimu wa muqawama na kusimama kidete katika kupigania haki zao.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *