Rdiamali ya Waziri wa Utamaduni wa Iran kwa hatua ya udhalilishaji ya jarida la Kifaransa

Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran ametoa radiamali yake kupitia ukurasa wake wa kijamii kuhusu hatua ya dharau na udhalilishaji iliyochukuliwa karibuni na jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo dhidi ya Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika toleo lake maalumu la siku ya Jumatano tarehe 4 Januari, jarida hilo la Ufaransa lilifanya kitendo cha kipuuzi cha kuanzisha shindano la kimataifa la michoro ya vikaragosi ambapo lilichapisha picha za kuudhi zilizoandamana na maneno na misemo michafu na ya matusi dhidi ya Kiongozi Muadhamu.

Waziri wa Utamaduni na Mungozo wa Kiislamu wa Iran, Mohammad Mahdi Esmaili, amejibu kitendo hicho cha kejeli na udhalilishaji cha jarida la Charlie Hebdo, kupitia ukurasa wake mtandaoni na kusema kumtusi kiongozi muhimu anayefutwa na mamia ya mamilioni ya watu walio huru na wanaopigania haki na ambaye kwa miaka sabini amekuwa akipambana dhidi ya dhulma, ukoloni na gaidi na hata kutoa mhanga afya na usalama wake kwa ajili ya kutetea uhuru wa watu wa Iran na taifa la Kiislamu, ni moja ya ishara na matokeo ya wazi ya mashine ya kuchochea chuki ya ustaarabu wa kinyama wa nchi za Magharibi.

Kufuatia hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kukashifu na kuvunjia heshima wanazuoni, matukufu na thamani za kidini na kitaifa za Iran, balozi wa Ufaransa mjini Tehran aliitwa jana Jumatano katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ili kubainishiwa malalamiko ya Iran kuhusu kitendo hicho cha dharau.

Nasser Kan’ani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameifahamisha serikali ya Ufaransa kuhusu malalamiko makali ya Tehran na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haikubali kutusiwa matukufu na thamani zake za Kiislamu, kidini na kitaifa. Ameongeza kuwa Ufaransa haina haki ya kutusi matukufu ya nchi nyingine na hasa mataifa ya Kiislamu kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *