Nchini Jamhuri ya Kiidemokrasia ya Congo, walinda amanii walipambana na raia na kulazimika kuondoka katika nchi hiyo. Na pia hiyo sio nchi pekee ya Kiafrika wanayoondoka.
Ripotii zinasema kuwa, jumbe za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zimepambana mwaka 2023 kuwalinda raia na kupata mafanikio madogo katika kuleta utulivu katika nchi wanazoendesha shughuli zao hasa barani Afrika.
Katika nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Sudan Kusini, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamepata mafanikio madogo mno kinyume na matarajio yaliyokuwako.
Kulingana na baadhi ya wachambuzi, vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyofanya kazi chini ya miongozo mikali vimeelemewa katika baadhi ya nchi hizo.
Mfano wa wazi ni Mali, ambako hali ya usalama haijatengemaa kwa sababu siku baada ya siku ghasia zinaonekana kuwa mbaya zaidi,” Adib Saani, mkurugenzi wa Kituo cha Usalama wa Binadamu na Ujenzi wa Amani cha Jatikay, ameziambia duru za habari. Ameongeza kusema kuwa, inaonekana kana kwamba ujumbe wa UN hauna msaada.”
Kwa wachambuzi kama Saani, utendaji duni wa hivi karibuni wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika baadhi ya maeneo ya Afrika unakatisha tamaa.
“Wameshindwa mara kwa mara kukabiliana na mzunguko wa vurugu katika nchi hizo na sababu yenyewe ya kuletwa hapo awali,” Saani alisema.