Ripoti: Mwaka 2022 umeshuhudia jinai kubwa zaidi katika historia ya Saudi Arabia

Mwaka huu unaomalizika wa 2022 unaelezwa kuwa, umeshuhudia ukiukaji wa haki za binadamu na jinai kubwa zaidi katika historia ya Saudi Arabia.

Ripoti ya Kanali ya Televisheni ya al-Alam iliyotolewa leo inaeleza kuwa, katika mwaka huu unaomalizika wa 2022 nchini Saudia kumeshuhudiwa ukiukaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu, jinai na utekelezaji wa hukumu za kunyonga watu kwa kiwango kikubwa mno ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusiana na haki za binadamu nchini Saudia ambapo sambamba na kuthibitisha kuendelea kukiukwa pakubwa haki za binadamu katika nchi hiio limetahadharisha juu ya kutokea jinai za kutisha katika mwaka ujao wa 2023.

Imekuja katika ripoti hiyo kwamba, matukio ya mwaka huu nchini Saudia kama hukumu za kunyonga ambazo hazijawahi kushuhudiwa, kufungwa magereza wanaharakati na kupigwa marufuku kusafiri nje ya nchi wapinzani wa nchi hiyo kiwango chake kinaweza kulinganishwa na matukio kama hayo lakini yaliyotokea na kurekodiwa nchini humo katika kipindi cha karne moja.

Ripoti za wataalamu wa mambo zinaonyesha kuwa, kabla ya mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo Muhammad bin Salman kushika hatamu za uongozi, Saudia ilikuwa nchi ya ukandamizaji; lakini baada ya mwanamfalme huo kuchukua usukani wa uongozi mwenendo wa ukandamizaji umeshadidi katika nchi hiyo kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa na kuifanya nchi hiyo kuwa katika safu ya nchi zinazoongoza kwa kukiuka haki za binadamu.

Tags

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *