Ripoti ya kulengwa kwa meli iliyopo kaskazini mwa Djibouti

Vyanzo vya habari vya Uingereza vilisema  kwamba meli ya kibiashara ililengwa na ndege isiyo na rubani katika maji katika masafa ya kilomita 110 kaskazini mwa Djibouti.

Siku ya Jumanne asubuhi, vyanzo vya ndani viliripoti tukio la usalama kwa meli katika eneo la mlango bahari la “Bab Al-Mandab”.
Shirika la Usafiri wa Majini la Uingereza limesema katika taarifa yake kwamba limepokea ripoti za shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye meli ya kibiashara katika maji kilomita 110 kaskazini mwa Djibouti.
Kampuni ya Embry Maritime Security pia ilitangaza kwamba meli hii iliyobeba bendera ya Visiwa vya Marshall ilipata uharibifu wa nyenzo kutokana na kugongwa na ndege isiyo na rubani.
Kabla ya hapo, Brigedia Yahya Saree, msemaji wa Jeshi la Yemen alitangaza Jumatatu jioni kwamba meli mbili za Marekani zililengwa katika operesheni mbili katika Ghuba ya Aden.
Kufuatia kushadidi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza, wanajeshi wa Yemen hawajaruhusu meli zozote zinazohusiana na utawala huo na zile zinazoelekea Palestina inayokaliwa kwa mabavu kupita katika Bahari Nyekundu na mlango wa bahari wa Bab al-Mandab.
Katika kuendeleza uungaji mkono wake kwa Tel Aviv, Marekani imeunda muungano wa kukabiliana na jeshi la Yemen baada ya operesheni za Yemen dhidi ya meli za Kizayuni kushadidi, na kuivamia ardhi ya nchi hii mara kadhaa.
“Ali al-Qahum”, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya muqawama ya “Ansarullah” ya Yemen, alionya Jumapili asubuhi: “Msisitizo wa Marekani, Uingereza na Israel juu ya kuendelea uchokozi utasababisha kuenea kwa migogoro katika mkoa.”

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *