Russia imefichua kuwa Marekani inawasafirisha magaidi wa ISIS au Daesh kutoka Syria na kuwaingiza Ukraine

Idara ya Usalama wa Nje ya Nchi ya Russia- SVR RF- imesema kuwa, Marekani inatuma magaidi Ukraine kutoka Syria.

Taarifa ya SVR-RF imesema magaidi hao wa ISIS wamekuwa wakipata mafunzo maalumu katika kituo kimoja cha kijeshi kilicho Syria kinyume cha sheria na baada ya kupata mafunzo wanaepelekwa Ukraine.

Taarifa hiyo imesema: “Mwishoni mwa mwaka 2021, Marekani iliwaachilia huru wafungwa wakiwemo makumi ya magaidi wa ISIS, na miongoni mwao walikiwemo raia wa Russia na nchi za CIS. Watu hawa walipelekwa katika kituo cha kijeshi cha al Tanf kinachosimamiwa na Marekani ambapo wamepewa mafunzo maalumu ya mbinu za kigaidi za vita na wametumwa eneo la Donbass.”

Marekani imetuma askari wake mashariki na kaskazini mashariki mwa Syria kwa kisigizio cha kupambana na ugaidi. Syria inasema wanajeshi hao wa Marekani wako nchini humo kinyume cha sheria kwa lengo la kuwaunga mkono magaidi na kupora utajiri wa nchi hiyo.

Idara ya Usalama wa Nje ya Nchi ya Russia imesema tayari magaidi wengi waliotumwa Ukraine wameshauawa katika oparesheni maalumu ya jeshi la Russia nchini humo.

Alhamisi iliyyopita, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza kuwa Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Marekani imeanzisha kampeni ya kuwaajiri mamuluki waingie vitani Russia. Imedokezwa kuwa mamluki wa mashirika ya American PMCs Academi, Cubic, na Dyn Corporation wanapelekwa vitani Ukraine. Taarifa hiyo imesema wiki iliyopita pekee mamluki 200 kutoka Croatia waliwasilia Ukraine kupitia Poland.

Rais wa Russia, Vladimir Putin Alhamisi tarehe 24 Februari aliamuru operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo la Donbass kujibu ombi la msaada wa kijeshi kutoka kwa viongozi wa jamhuri za Donetsk na Luhansk huko Mashariki mwa Ukraine. Russia imekuwa ikilalamika kwa muda mrefu kuwa, serikali yenye misimamo ya kimagharibi ya Ukraine inalenga kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO unaoongozwa na Marekani na hilo ni tishio kubwa kwake.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *