Russia: Umoja wa Ulaya hauna uvumilivu katika suala la uhuru wa kutoa maoni

pika wa Bunge la Russia Duma ameushutumu Umoja wa Ulaya (EU) kwa kubana maoni mbadala na kuminya uhuru wa kujieleza kwa lengo la kuwahadaa raia.

Vyacheslav Volodin ameeleza hayo kufuatia marufuku ya hivi karibuni iliyopitishwa na Brussels kwa vyombo vya habari vya Russia na kuibua indhari za kujibu mapigo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia.
Siku ya Ijumaa, Baraza la Ulaya lilitangaza kuwa linasimamisha shughuli za utangazaji za mashirika manne ya ziada ya vyombo vya habari, likidai kwamba “vinaeneza na kuunga mkono” propaganda za Kirusi.

Orodha ya vyombo vya habari vilivyopigwa marufuku na Umoja wa UUlaya ni pamoja na wakala wa habari wa RIA Novosti, magazeti ya Izvestia na Rossiyskaya Gazeta, na tovuti ya habari ya Voice of Europe yenye makao yake nchini Czech.

Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, Volodin amesema hatua hiyo inaonyesha utashi ilionao EU wa “kufunga upatikanaji wa taarifa zisizo na upendeleo na za kuaminika” kwa wakazi wa nchi wanachama.

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge la Russia, sera ya undumilakuwili imekuwa sehemu muhimu ya miundo ya Ulaya kwa sababu EU inazungumza tu juu ya uhuru wa kutoa maoni, lakini katika uhalisia hawalivumilii jambo hilo.

Siku ya Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilitangaza kuwa, Moscow imeshauonya Umoja wa Ulaya mara kadhaa kwamba hatua kandamizi dhidi ya vyombo vya habari vya Russia hazitaachwa bila kujibiwa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Russia Maria Zakharova alitangaza kuwa kupuuza maonyo hayo kutailazimisha Moscow kuchukua hatua za kujibu mapigo ambazo hazitaweza kuepukika…

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *